Responded HOJA Walimu wa kujitolea Shule za Msingi, Sekondari - Morogoro waboreshewe maslahi, malipo hayaendani na hali halisi ya sasa

Responded HOJA Walimu wa kujitolea Shule za Msingi, Sekondari - Morogoro waboreshewe maslahi, malipo hayaendani na hali halisi ya sasa

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Licha ya mahitaji makubwa ya walimu kwa Shule za Msingi na Sekondari, bado walimu wanaojitolea wanaishi maisha magumu, kwa kukosa posho na wengine wakiambulia kulipwa Sh 100,000 kwa mwezi.

Takwimu za BEST (Basic Education Statistics Tanzania) zinaonesha Tanzania inakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu, ambapo hadi Mwaka 2023, waliokuwa wameajiriwa walikuwa 84,700 na mahitaji yalikuwa walimu 89,932 sawa na asilimia 51.5.

Kwa shule za msingi Walimu waliojiriwa ni 180,325 mahitaji ya Walimu wa Shule za Msingi ni Walimu 366,650, hivyo kuna uhaba wa walimu 186,325.

Stella Mpangala (sio jina lake halisi) amekuwa akitolea katika Shule ya Sekondari Kimamba iliyopo Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro tangu Mwaka 2022.

“Mimi ni mwalimu mwenye diploma ya elimu, nilianza kujitolea tangu Mwaka 2022. Wakati huo tulikuwa walimu wanne na wote tulikuwa hatulipwi chochote. Baada ya mwaka mmoja wenzangu watatu waliondoka baada ya kuona maisha ni magumu, mimi nikaendelea kuwepo. Mwaka 2025 aliyekuwa mkuu wa shule alistaafu, akaletwa mwingine,” anaeleza.

Anasema ili kujikimu kimaisha alikuwa akiuza maandazi kwa wanafunzi huku shule ikimpatia chumba cha kuishi. Baada ya mkuu wa shule wa awali kustaafu, anasema alikutana na mkuu mpya na kumweleza shida yake.

“Ndipo alipoitisha kikao cha kamati ya shule na alinialika. Baada ya kujadiiana na kamati, ikaonekana kuna nafasi ya matroni, ndipo wakanishauri pamoja ualimu, niwe matroni ili nilipwe, nikakubali. Malipo yenyewe yakawa ni Sh 100,000. Tunaolipwa hivyo ni mimi, wapishi wawili, sektretari na wallinzi watatu,” anasema na kuongeza, “Tangu nimekuwa matroni, nalala kwenye bweni la wanafunzi.”

Pia soma ~ Wanu Ameir: Halmashauri ziendelee kutenga fedha kuwalipa Walimu wa Kujitolea

Hata hivyo, anasema mwanzo wa mwezi huu (Mei), ambapo mkuu wa shule alimwita tena akasema atamwongeza Sh 50,000 lakini wakati wa kusaini malipo ajaze kwamba yeye ni mpishi, kwa sababu hela zenyewe zinatoka kwenye bajeti ya chakula.

Mbali na mwalimu huyo, uchunguzi umeonyesha zipo shule nyingine pia zinalipa Sh 100,000 kwa walimu wanaojitolea, zikiwamo shule za Mkoa wa Pwani.

“Kwa mfano hapa shuleni kwetu kuna walimu wawili wanalipwa Sh 100,000 kwa mwezi. Malipo hayo hutokana na michango ya walimu na wakati mwingine michango ya wazazi,” alisema mwalimu mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina wala shule anayofanyia kazi.

“Hakuna sheria wala mwongozo unaoelekeza malipo ya walimu wa kujitolea, ni suala tu la mkuu wa shule anapoona kuna mahitaji ya walimu ndio wanawachukua na anaangalia uwezekano wa kuwalipa,” anaongeza.
 
Wakati mbunge Day yake pale mjengoni ni laki 3.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom