Edsger wybe Dijkstra
JF-Expert Member
- Aug 22, 2019
- 244
- 491
Wadau niaje, mimi ni mwalimu wa sekondari wa hesabu na physics, sasa hapa katikati nilihamia mikoa ya kusini, ikabidi nianze upya process za kutafuta kazi.
Asee kwa kuwa maisha hayasubiri nikasema nisichague kazi , nilitonywa na mwana kuwepo kwa nafasi ya ualimu english medium shule moja maaarufu jijini mbeya. Si nikatimba kwenye written interview.
Ah we picha linaanza mtihani maswali ni ya kujumlisha , kuzidisha , sehemu, takwimu kidgo na geometry ( maumbo).
Nikapiga maswali yote chap chap baada ya dakika 15 nikatoka maticha ya primary yakabaki yanashangaa.
Aroo matokeo kutoka nimepata 45 ya 45 ila naambiwa sipewi kazi kwa kuwa sijaonyesha njia vizuri 😂😂😂😂
Yani kugawanya mpk uonyeshe unavyoteremsha kila namba , unavyoongeza zero baada ya desimali nk yani kila hatia uoneshe kwenye karatasi ya majibu .aaaah kama ualimu wa primary ndo ivo aisee kazi mnayo! Poleni Sijapata ona!!