Walimu wa Sekondari kusimamia Mitihani ya Darasa la 7.

Walimu wa Sekondari kusimamia Mitihani ya Darasa la 7.

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
Wana JF je, hizi tetesi za walimu wa sekondari kusimamia mitihani ya darasa la saba ni za kweli? na kama ni kweli lengo ni nini?
 
Hiyo sio tetesi ni kweli waziri wa Elimu Mh. Kawambwa amelieleza bungeni kupitia kauli za mawaziri. Alisema sasa hivi mitihani ya darasa la saba itakuwa na MSIMAMIZI MKUU ambaye atakuwa mwalimu wa sekondari. Kwa hiyo kutakuwa pia na wasimamizi wadogo kama zamani.
 
lengo lao nn? Hawajamaa wanafanya siasa maisha ya watoto masikini wananikera kiukweli,badala ya kujadili jinsi ya kuongeza walimu na kuboresha shule za kata wanakuja na ujinga wao,unajenga choo wakati hujui utakula nn??
 
Kwa mawazo hayo finyu kweli uwezo wa kufikiri wa waziri Kawambwa umefika mwisho. Tunaitahadharisha serikali iache kuchezea walimu wa shule za msingi ambao ndiyo waliotufikisha hapa. kama ni hivyo basi wafundishe hao walimu wa shule za sekondari. Walimu wametoka kwenye mgomo hata hawajaisha wanakuja na tamko la kitoto. Huyo Kawambwa kashindwa hata kusimamia miundombinu leo kapewa elimu kweli watanzania tunapelekeshwa.
 
Back
Top Bottom