KERO Walimu wa Shule ya Shekilango Sinza wanang'ang'ania kutoa watoto wa la saba saa 1 usiku. Wizara tusaidieni kukomesha hii

KERO Walimu wa Shule ya Shekilango Sinza wanang'ang'ania kutoa watoto wa la saba saa 1 usiku. Wizara tusaidieni kukomesha hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakuu,

Kuna ndugu yangu wangu la 7 ndo anarudi shule leo karudi saa 1 usiku. Muda wa kutoka shule ni saa 10 lakini hawa la 7 wanakalishwa hadi saa 1 usiku

Nilivyouliza kwanini wanabaki hadi muda huo nimeambiwa wanasoma masomo ya ziada ili kujiandaa na mtihani wa taifa. Lakini kwenye kubaki huko wanachangia mia 5 ya masomo na mia 5 ya uji. Hili sio tatizo kabisa lakini issue ni hapo kwenye kutoa watoto saa moja usiku

Huyu ndugu yangu yeye huwa anaamka saa 11 maana wanawahi kuingia darasani saa 12 asubuhi. Yaani mtoto anatoka nyumbani saa 11 asubuhi anafika nyumbani saa 2 usiku na wale wanaokaa mbali hadi saa 3 usiku. Kweli? Ni masomo gani ya hivyo jamani?

Nawaomba sana mpaze sauti ili Wizara ya Elimu itoe tamko la kustopisha hili suala mara moja. Wezi, vibaka, nk

Usiku una mambo mengi lakini walimu hawaelewi. Nashindwa kumtoa mwanangu kwa sababu kuna wazazi wachache wanapenda huu mfumo

Tusaidieni. Shule ni Shekilango iko Sinza
 
Huu ujinga umetoka na ukosefu wa Elimu kwa Wazazi kwa asilimia 70,
Wanapokua kwenye vikao wao kazi yao ni ndio mwalimu,
hawajui kujenga hoja wala kupinga hoja,

Tunawatakia masomo mema wanafunzi hao 😎😎.
 
Huu ujinga umetoka na ukosefu wa Elimu kwa Wazazi kwa asilimia 70,
Wanapokua kwenye vikao wao kazi yao ni ndio mwalimu,
hawajui kujenga hoja wala kupinga hoja,

Tunawatakia masomo mema wanafunzi hao 😎😎.
Kuna mtoto anamaliza darasa la saba na mimba juuu
 
Zamani sisi tulikuwa tunatoka shule saa nane na hakuna kurudi hadi kesho ila tulifauru vizuri tu
Taifa la sasa limejaa matapeli tu waalimu wasiona weledi wa kufundisha wao nikuwaza tarehe za mshahara tu
 
Lsasa najiuliza hata hiyo akili si inachoka?
Hao walimu hawana lolote wanataka hivi vi 500 kama wanaweza wafanye bure!
 
Huu ujinga umetoka na ukosefu wa Elimu kwa Wazazi kwa asilimia 70,
Wanapokua kwenye vikao wao kazi yao ni ndio mwalimu,
hawajui kujenga hoja wala kupinga hoja,

Tunawatakia masomo mema wanafunzi hao 😎😎.
Nakazia hoja: Halafu hao-hao wazazi walioitika ndio mwl. leo wanakuja na hoja ya watoto wanatoka saa 1 usiku kana kwamba hawakuwepo kwenye kikao.
 
Juzi nimemmaindi mwl mkuu wa shule anayosoma binti yangu. Yeye anagraduate mwaka huu.

Juzi mtoto amerudi shule saa mbili usiku. Siku zote huwa saa 12 na nusu anakuwa ashafika home baada ya masomo ya ziada kwa drs la saba.

Namuuliza mtoto mbona kuchelewa Leo, ananijibu eti amechaguliwa kundi la ku dance kwaajili ya siku ya graduation so wanafanya rehearsal kuanzia saa 12 mpaka saa 1:30.

Nikampigia mwalimu mkuu kumuuliza kulikoni, then nikamwambia kama hawataangalia namna ya kubalance vzr mda wa watoto kurudi nyumbani mwanangu hatoshiriki hiyo michezo. Siku ya pili akarudi muda wa kawaida.

Walichofanya rehearsal wamepanga kufanya mara mbili kwa wiki na wanaanza saa kumi jioni.
 
Safi sana na changamoto imepata ufumbuzi chap' badala ya kukalia kuleta kero humu.
 
Back
Top Bottom