Walimu wa Tanzania wako wapi? au wao wana maisha mazuri sana? Kenya wanakiwasha

Tujilinganishe na Marekani au China? Kenya ndio size yetu
 
Walimu wa Tanzania ni Kama watanzania wengine tu maana hata mimi na wewe hapo life ikiwa haieleweki hatuwezi kukiwasha. Kenya ni level nyingine maana wao hawakuanza Jana wala juzi na Chama chao cha walimu kimewahi kujinasibu kuwa kina uwezo wa kuwalipa walimu mshahara kwa muda flan Kama serikali itakataa kuwalipa sababu ya mgomo labda.
Tanzania Chama Cha walimu ili tu kinunue Gari la maafa na starehe wilaya labda ni lazima lizuie gawio linaloenda kwenye matawi yake wilayani hapo😀
Hapa walimu mtawatwisha tu mzigo ila watanzania wote tu ni watu aina ya walimu
 
Wako bize kugombani ukatibu Elimu wa Kata
 
Na ndivyo ilivyo.....wanapenda uhuru. Na maboss nao wanawajua kuwanyonya watumishi kupitia hiyo loophole
 
Wakenya wanajielewa sio matz mengi ni Mazezeta, hujui aliyesoma na asiyesoma! Tatizo la tz ni mwenge!!!
 
Sasa wewe usie na mnyororo si uingie barabarani tukuone ili sisi watumwa tukufuate?

Yaan kila kitu tunataka tujifananishe na Kenya hiyo sio sawa

Wa bongo wamepewa hadi Vishikwambi wstaje nini tena?! 😆😆
 
Wahamie Kenya ili mmbaki mazombie tu hapa Tanzania?
 
Walimu wetu ni mabilionea ndio maana walichanga fomu ya rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…