hata anayebisha ameshazoea kupinga tu ila walimu wa vyuo vikuu nchini kote walio wengi wanajifanya miungu watu, kwa kuwa test, UE wanatunga wao na kusahihisha wao. Kuna mwalimu mmoja mhaya chuo kimoja pale morogoro nahisi ye ndo mungu wa wanafunzi anaowafundisha.
Kama unaamini umeonewa na huyo mwalimu kama unavyodai unayo nafasi ya kwenda kulalamika kwa mkuu wa idara husika hilo somo linapofundishwa kwa sababu mkuu wa idara ndiye msimamizi mkuu wa masomo katika idara yake na anayo mamlaka ya kuangalia iwapo malalamiko yako yana ukweli na iwapo ataona yana ukweli anaweza kumwajibisha mwalimu huyo kwa kufuata ngazi za kimamlaka za nidhamu za chuo.
Iwapo hutaridhika unaweza kumuona Dean ambaye ndiye afisa taaluma mkuu wa kitivo chako na iwapo kama hutaridhika na maamuzi ya Dean unaweza kwenda mbele zaidi kwa makamu wa chuo anayeshughulika na taaluma.
Pia iwapo maamuzi ya makamu wa chuo-taaluma hutaridhika nayo, kwa kushirikiana na uongozi wako wa wanafunzi unaweza kukata rufaa kupinga matokeo kwa baraza la seneti na baraza la seneti likiona unayo hoja lina uwezo wa kuamuru mitihani yako ikasahihishwa upya na mwalimu mwingine wa taaluma husika ndani au nje ya chuo chako bila mwalimu wa awali kuhusishwa.
Kumbuka pia kwamba baraza la seneti lina wajumbe kutoka nje ya chuo na pia wanafunzi wanao uwakilishi.
Ngazi zote hizo zimewekwa ili kutoa haki na kulinda ubora wa taaluma.
Kwa taratibu za chuo si rahisi kwa mwanafunzi kufeli kwa kuonewa kama mwanafunzi amefeli amefeli kweli.
Ni vema kujua pia wapo wengi waliofeli masomo yao chuoni lakini wanafanya vema katika tasnia mbali mbali za kimaisha.
Kama si mwanafunzi au ndugu yako ndo kafeli kakudanganya kwamba kaonewa, Nakushauri uache kupoteza muda kuchafua watu kwa kitu usichokijua badala yake mpe ushauri chanya nduguyo
Katika vyuo vinavyojali ubora wa taaluma hakuna njia mkato, bidii yako ndio mafanikio yako.
Wasalaam
Mtu Mzima