Walimu wa vyuo vikuu wapunguziwe mamlaka kwa wanafunzi wanao wafundisha

Baadhi ya wahadhiri wanaamini watu wa makabila yao wana akili sana na hivyo hawatakiwi kufeli na hili nimeshuhudia mwenyewe mf.wahaya na wachaga.Yuko mhaya mmoja mwenye asili ya Rwanda,yeye ni mkuu wa chuo fulani,akipita mnywarwanda hapo ama mhaya lazima wafaulu hata kama ni kwa kampeni chafu.Kuna mchaga mmoja ni associate prof kwa sasa yuko chuo kimoja dodoma,hafai kuwa hapo kabisa kutokana na faulo anazocheza kwa kugawa alama za juu kwa wachaga wenzie hata kama ni vilaza. Watu kama hawa hunifanya nichukie sana kuwa mtanzania

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Mkuu nakuunga mkono kabisa na mimi nimekuwa nikisema ikitokea nimeulizwa unapenda nini kifanyiwe marekebisho ningesema mfumo wa vyuo vikuu walimu kuwa na mamlaka makubwa. Kuna vyuo vyenye mlengo wa kiccm ukijulikana tu we kamanda active umepote..na tumewapoteza wengi atabisha ambaye hayajamkuta nashangaa hata hako kada kanaitwa Radhia Sweety kanabisha sijui kanamatatizo gani hako kadada hapo hata boyfriend wake anashida kuwa na mtu wa kupinga pinga hata kama jambo hakajalielewa
 
hata anayebisha ameshazoea kupinga tu ila walimu wa vyuo vikuu nchini kote walio wengi wanajifanya miungu watu, kwa kuwa test, UE wanatunga wao na kusahihisha wao. Kuna mwalimu mmoja mhaya chuo kimoja pale morogoro nahisi ye ndo mungu wa wanafunzi anaowafundisha.
 

Kama unaamini umeonewa na huyo mwalimu kama unavyodai unayo nafasi ya kwenda kulalamika kwa mkuu wa idara husika hilo somo linapofundishwa kwa sababu mkuu wa idara ndiye msimamizi mkuu wa masomo katika idara yake na anayo mamlaka ya kuangalia iwapo malalamiko yako yana ukweli na iwapo ataona yana ukweli anaweza kumwajibisha mwalimu huyo kwa kufuata ngazi za kimamlaka za nidhamu za chuo.

Iwapo hutaridhika unaweza kumuona Dean ambaye ndiye afisa taaluma mkuu wa kitivo chako na iwapo kama hutaridhika na maamuzi ya Dean unaweza kwenda mbele zaidi kwa makamu wa chuo anayeshughulika na taaluma.

Pia iwapo maamuzi ya makamu wa chuo-taaluma hutaridhika nayo, kwa kushirikiana na uongozi wako wa wanafunzi unaweza kukata rufaa kupinga matokeo kwa baraza la seneti na baraza la seneti likiona unayo hoja lina uwezo wa kuamuru mitihani yako ikasahihishwa upya na mwalimu mwingine wa taaluma husika ndani au nje ya chuo chako bila mwalimu wa awali kuhusishwa.

Kumbuka pia kwamba baraza la seneti lina wajumbe kutoka nje ya chuo na pia wanafunzi wanao uwakilishi.

Ngazi zote hizo zimewekwa ili kutoa haki na kulinda ubora wa taaluma.

Kwa taratibu za chuo si rahisi kwa mwanafunzi kufeli kwa kuonewa kama mwanafunzi amefeli amefeli kweli.

Ni vema kujua pia wapo wengi waliofeli masomo yao chuoni lakini wanafanya vema katika tasnia mbali mbali za kimaisha.

Kama si mwanafunzi au ndugu yako ndo kafeli kakudanganya kwamba kaonewa, Nakushauri uache kupoteza muda kuchafua watu kwa kitu usichokijua badala yake mpe ushauri chanya nduguyo

Katika vyuo vinavyojali ubora wa taaluma hakuna njia mkato, bidii yako ndio mafanikio yako.

Wasalaam
Mtu Mzima
 
we kinachokushinda kutaja mzumbe ni nini? nyie wanafunzi ndo mlikua vihereehere. na habari yako umeipindisha kuficha ukweli..tatizo lenu weng LLB mlikua mnakesha na kushinda bar halafu mnalazimisha kupata A nani aliwaambia mzumbe ni casino?

heeee....kumbeeeeeee
 




Kama chuo hicho ni SUA wala si ajabu. Kuna Prof wa Engineering alikula kichwa cha mwanaye (alim-Disco)tena wa kumzaa sembuse mtu baki ndiyo aachiwe!! Chezea Sokoine University of Assignments weweee????
 
Funguka zaidi,vinginevyo husomeki ... inaonekana una point ila umeshindwa kuiweka sawa sawa

Nautafel sana,maana ujitambui kwan chuo umeenda kuxoma au mapenzo,NI MARUFUKU KWA MWANAFUNZI( Chekechea,mcng,sec,na chuo kufanya mapenz) ondoa pumba zako
 
Nautafel sana,maana ujitambui kwan chuo umeenda kuxoma au mapenzo,NI MARUFUKU KWA MWANAFUNZI( Chekechea,mcng,sec,na chuo kufanya mapenz) ondoa pumba zako

dah!!! siamini kama great thinker anaweza toa view kama hii!!

hivi haujui vyuoni tuna wake zetu na familia zetu tunasoma nazo?

serikali iko responsible kwa watoto wa chekechea mpaka form six tu!!

kajipange upya kijana!!
 

inauma sana bro!!!

lakini kwa upande mwingine wanafunzi nao wanachangia sana kufeli ama kufaulu kwao!!

hujaona madem wanavyojiuza kwa walimu wao ili wafaulu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…