Walimu wa Zamani hawataki kubadilika kuendana na mtaala mpya.

Soul21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
210
Reaction score
351
Ninaandika haya kama ajira mpya lakini mwenye uzoefu mkubwa katika ufundishaji.
Nimefika kwenye kituo cha kazi shule ya sekondari na nilichokutana nacho nitofauti na matarajio ya waziri wa elimu.
Walimu waliopo kazini muda mrefu bado wameshikilia mifumo ya ufundishaji wa zamani yaani kujaza ubao maandiko bila kutoa uhuru wa mawazo na michanganuo kwa wanafunzi.
Kutokana na haya nimeona kuwa bado somo la Kiswahili halitazalisha wataalamu wa fasihi na kufanya tasnia yetu ya sanaa kukua kwa sababu wanafunzi wanakariri kuliko kufanya vitu.
Pili, Bado wahitimu wa kidato cha nne hawataweza kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza ipasavyo kwa sababu wanaandika zaidi ya kuwasiliana. Yaani wapo kwenye mfumo wa zamani wa kusoma notes ili kujibu mtihani hali inayopelekea wanafunzi kuwa na taarifa kuliko maarifa.
Tatu, Kama ufundishaji wa kutoa notes utaendelea licha ya serikali kutoa vitabu vya kutosha basi wataalamu wa sayansi watendelea kubaki na taarifa ambazo hazita tatua changamoto halisi za watanzania.
Nahimiza walimu wenzangu kuwa, tusiwaumize hawa watoto kama tulivyoumizwa sisi bali tukubali kubadilika ili tuwe chachu ya maarifa kwa masomo yote na kujenga kizazi cha kufikiria na kutatua changamoto.
Ajira mpya wamekuja na ubunifu ila walimu wachache sana wapo tayari kubadilisha uzoefu na ajira mpya.
Ajira mpya sio tishio la nafasi yako bali yeye ni sehemu ya ukuaji wa elimu ya Tanzania, tubadilishane maarifa.
 
Mwalimu mpya mwenye uzoefu "mwingi" kuliko uliowakuta wapo miaka salasini na tisa?Sisi tulifundishwa na walimu wa Universal Primary Education na tukawa very brights.Acha sound nyingi,tupe matokeo chanya.Teaching an old dog the new tactics of hunting!
 
Kuwe na viongozi wa juu wanao evaluate ama inspect utoaji wa hio elimu. Kama wanafunzi wanapata kile kinachopaswa kuwa. Pia hao walimu wanafanya wanayofanya sababu hamna anayewafanya accountable...kungekuwq na inspector anayewacheki regularly wasingefanya ujinga wanaofanya..
 
Kumbe ndio maana madaftari hayajai ila yanachoka tu.!

Mnaona tabu kuwaandikia mnawapigisha stoli mkimaliza mnawaambia kesho waje na bukubuku za mtiani

Madaftari ya mazoezi hayasahihishwi yanavinotsi kidogo tu vya ushahidi

Tena kwa niaba ya wazazi wenzangu wa kayumba huo mtindo wenu wakuhamisha mazoezi kutoka kwenye madaftari na kuyaita mitihani ya kila baada ya siku mbili tumeuchoka

Mnaona bora kukopi vikarasi vingi na kufanya biashara ya kuibia wazazi pesa zao kuliko kuwajibika kwa chaki na ubao

Leo ndio Nimejua tena Ahsante kwa taarifa
 
Wazee sugu!! Kanyaga twende!!
Kazi ni kipimo cha utu
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ninaandika haya kama ajira mpya lakini mwenye uzoefu mkubwa katika ufundishaji.
Nimefika kwenye kituo cha kazi shule ya sekondari na nilichokutana nacho nitofauti na matarajio ya waziri wa elimu.
Walimu waliopo kazini muda mrefu bado wameshikilia mifumo ya ufundishaji wa zamani yaani kujaza ubao maandiko bila kutoa uhuru wa mawazo na michanganuo kwa wanafunzi.
Kutokana na haya nimeona kuwa bado somo la Kiswahili halitazalisha wataalamu wa fasihi na kufanya tasnia yetu ya sanaa kukua kwa sababu wanafunzi wanakariri kuliko kufanya vitu.
Pili, Bado wahitimu wa kidato cha nne hawataweza kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza ipasavyo kwa sababu wanaandika zaidi ya kuwasiliana. Yaani wapo kwenye mfumo wa zamani wa kusoma notes ili kujibu mtihani hali inayopelekea wanafunzi kuwa na taarifa kuliko maarifa.
Tatu, Kama ufundishaji wa kutoa notes utaendelea licha ya serikali kutoa vitabu vya kutosha basi wataalamu wa sayansi watendelea kubaki na taarifa ambazo hazita tatua changamoto halisi za watanzania.
Nahimiza walimu wenzangu kuwa, tusiwaumize hawa watoto kama tulivyoumizwa sisi bali tukubali kubadilika ili tuwe chachu ya maarifa kwa masomo yote na kujenga kizazi cha kufikiria na kutatua changamoto.
Ajira mpya wamekuja na ubunifu ila walimu wachache sana wapo tayari kubadilisha uzoefu na ajira mpya.
Ajira mpya sio tishio la nafasi yako bali yeye ni sehemu ya ukuaji wa elimu ya Tanzania, tubadilishane maarifa.
Teaching is a noble profession.

Chief Nanga.
 
Kuwe na viongozi wa juu wanao evaluate ama inspect utoaji wa hio elimu. Kama wanafunzi wanapata kile kinachopaswa kuwa. Pia hao walimu wanafanya wanayofanya sababu hamna anayewafanya accountable...kungekuwq na inspector anayewacheki regularly wasingefanya ujinga wanaofanya..
Unaelewa kama kuna watu wanaitwa wadhibiti ubora wa elimu?
 
Back
Top Bottom