Walimu waajiriwa wa 2011 tukutane hapa, Serikali imetusahau

Ramea

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
2,146
Reaction score
4,084
Ndugu walimu na wakufunzi wa shule za sekondari na vyuo tulioajiriwa 2011, tupeane machache hapa kuhusu hatma yetu ya kupanda madaraja kadiri ya taratibu za kiutumishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2015.

Kiutaratibu tulitakiwa kupanda madaraja july 2014 lakini serikali kupitia TAMISEMI, Ilisema intake hii ya waajiriwa itapandishwa madaraja ifikapo july 2015. Nakumbuka naibu waziri TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mh. Kassim Majaliwa alitembea mikoa mbalimbali Tanzania na katika ziara hii alithibitisha hili kwenye mikitano yake na walimu nchi mzima.

Cha kushangaza hadi leo halmashauri nyingi hazijatoa barua za kupandisha madaraja hadi sasa na haijulikani kama july hii tutapata mishahara mipya au la. Nadhani tunachezewa danadana na sababu za kutotoa barua had sasa ni zipi? kuna kitu hapa. Maana kuwa nayo tu ile barua hata mshahara usipobadilika, kuna faida kubwa kiutumishi.

Naomba tuutumie uzi huu kujuzana kama kuna halmashauri zilizotoa barau had kufikia leo hii.

KARIBUNI.
 
Bora mkutane na viele ele vyenu kila kukicha shida zenu zinaongezeka na mwaka huu mchague tena ccm mtakoma.

swissme
 
Bora mkutane na viele ele vyenu kila kukicha shida zenu zinaongezeka na mwaka huu mchague tena ccm mtakoma.

swissme

mbona baba ako ana chagua Ccm na bado. shida. zake anazo au unazan walimu Wote wapo Ccm kuwa na akil kidogo bint yangu
 
mbona baba ako ana chagua Ccm na bado. shida. zake anazo au unazan walimu Wote wapo Ccm kuwa na akil kidogo bint yangu
Baba yangu ukawa.nyie walimu mnalala chini na kushinda kuitisha watoto wa watu michango ili mule kila siku matatuzo na ukifika uchaguzi ccm wanawavalisha kofia na kanga kisha mnasahau kila kitu kwa wali na kupigia ccm kura.ccm wanawata nyie eti misukule ya ccm.na elimu yenu.fungukeni


swissme
 
Kwani July imeshafikaa?

Barua za kutaarifiwa kupanda daraja zinatolewa kuanzia march/april. July unakutana na ongezeko la mshahara kwenye account yako.
 
Barua za kutaarifiwa kupanda daraja zinatolewa kuanzia march/april. July unakutana na ongezeko la mshahara kwenye account yako.

Daa poleni sana!! Vumilieni tuu maana serikali yetu sikivu itakua imeliona hili
 

Wakuu mnaharibu uzi, siyo lazima mbishane kwenye uzi huu.
 
Nani alikuambia unapaswa kupanda 2013 wakati imeanza kazi 2011? Kumbuka unapanda daraja baada ya miaka3, ila kwa ajira mpya Kuna mwaka 1 WA probation kabla hujathibitishwa Kazini so ilipaswa upande baada ya miaka 4
 
Nani alikuambia unapaswa kupanda 2013 wakati imeanza kazi 2011? Kumbuka unapanda daraja baada ya miaka3, ila kwa ajira mpya Kuna mwaka 1 WA probation kabla hujathibitishwa Kazini so ilipaswa upande baada ya miaka 4

Hakuna ilipoandikwa 2013 kwenye mada hii.
 
Kama uliajiriwa 3/2011

3/12 kuthibitishwa kazini
3/13 mwaka wa kwanza
3/14 mwaka wa pili
3/15 mwaka Watatu (you deserve promotion ). Ila kwa bahati mbaya mwaka wa fedha 2015/2016 wanapandisha walimu waliokua wamefika ukomo baada ya madaraja yao kufunguliwa
 

Uzi haukuhusu, michakato ilishafanyika. Hata kuhakiki majina ya watakaopanda 2015/2016 yalisambazwa shuleni kuanzia march na tunajijua ila tatizo ni barua tu. Usiandike kitu usichokijua, nani kakuambia 2011 tuliajiriwa mwez wa 3?. Serikali yenyewe inajua kuwa mwaka jana hakupandisha madaraja ndiyo maana ilitoa tamko na kututaka tuwe wavumilivu hadi mwaka huu.
Nyie ndiyo mnaojipendekeza bila kutambua haki zenu.
 

Yawezekana wilayani kwako mwaka Jana hawakupandisha, ila nilipo Mimi wamepanda, pia Kama Majina ya Promo yameshatoka Si usubiri barua? Vikao vingi Promo ya mwaka huu vimekaa kati ya April -June

Halafu Nliposema 3/2011 sikumaanisha lazima Uwe umeajiriwa March, nlitaka kuonesha mwaka na Mwezi WA ajira Hadi Promo,


pia usiwe mkali mkuu Kama unataka kujua
 

Teh Tehe Teh! kumbe na wewe ni mwalimu. Hahahahaaa! nilijua nachati na mwakilishi wa TAMISEMI. LOL
 
Toeni povu tu. nadhani serikali yenu mnaijua.kupanda madaraja sio lelemama.
 

acha dharau
 
ndyo kuna baadhi ya watu walopangwa mikoa ya pembezon walipanda tangu mwaka Jana; ila kwa mikoa yenye walimu wengi bado cjaona kama wamepewa barua' ila mchakato unaendelea kwa hyo barua zitatoka
 
walimu kweli mna matatizo makubwa ya kiakili, kwani simeahidiwa JULY, sasa mbona mshaanza kulialia na wakati julai yenyewe haijafika.
Hebu kafundishe huko acha kuwashushia hadhi walimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…