DOKEZO Walimu wadai Viongozi wa mageuzi ndani ya CWT wanapigwa vita

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

MNYONGE MIMI

New Member
Joined
May 26, 2026
Posts
1
Reaction score
1
Kuna jambo linaendelea ndani ya Chama cha Walimu Tanzania ambalo linaacha maswali mazito sana kwa walimu wengi na wananchi wanaofuatilia kwa karibu.

Kwa miaka mingi walimu walikata tamaa na chama chao. Chama kilionekana kuacha kabisa kazi ya msingi ya kutetea walimu na badala yake kikaanza kutumiwa na watu wachache kwa ajili ya maslahi binafsi. Ndani ya walimu kulikuwa na maneno mengi sana kuhusu fedha za makato ya asilimia 2% za walimu. Ilisemekana wazi kwamba kulikuwa na mtandao wa watu waliokuwa wakinufaika na fedha hizo kwa kiwango kikubwa sana.

Walimu wengi walikuwa wakisikia kwamba baadhi ya mawaziri, makatibu na watu wenye ushawishi wa kisiasa walikuwa wakipewa hadi zaidi ya milioni mia mbili kila mwezi, fedha ambazo kwa ujumla wake zilifika zaidi ya bilioni moja na nusu kila mwezi bila maelezo ya wazi kwa walimu wenyewe ambao fedha hizo zilikuwa zinakatwa kutoka kwenye mishahara yao.

Baadaye viongozi wachache ndani ya chama wakakataa kuendelea na mfumo huo. Wakaanza kuuliza maswali. Wakaanza kusimama kidete kusema haiwezekani fedha za walimu ziendelee kutumika kwa namna hiyo huku walimu wenyewe wakiteseka. Ndipo vita vikaanza.

Tangu mwaka 2023 na 2024 kulikuwa na figisu nyingi sana kuhakikisha viongozi waliotaka mabadiliko wanaondolewa. Lakini walimu wengi waliendelea kuwaunga mkono kwa sababu waliona kwa mara ya kwanza kuna watu wanataka chama kirudi kuwa sauti ya walimu.

Baada ya kuingia madarakani Dkt. Suleiman Ikomba, mwaka 2025/2026 chama kilianza kuonekana tofauti kabisa. Kero za walimu zikaanza kusikilizwa. Serikali na chama zikaanza kufanya kazi kwa karibu zaidi. Programu kama Samia’s Teachers Mobile Clinic zikaanza kuzunguka nchi nzima kutatua shida za walimu moja kwa moja.

Ndiyo maana leo walimu wengi wanaumia kumuona Dkt. Suleiman Ikomba akisukumwa kwenye kesi na misukosuko ya mambo ya zamani ambayo hata yeye mwenyewe hahusishwi moja kwa moja nayo.

Watu wanauliza maswali mengi:
  1. Kama kweli kuna haki, kwanini viongozi washikiliwe bila dhamana?
  2. Kwanini kesi za zamani zilizowahi kuchunguzwa na kufungwa zinafufuliwa tena leo?
  3. Kwanini jambo hili lifanyike kwa namna ambayo inaonekana lengo ni kuwatoa viongozi madarakani kwanza kabla ya ukweli kujulikana?
Walimu wengi wanaamini kuna watu wameguswa na kufungwa kwa mianya ya fedha na maslahi yao binafsi, ndiyo maana vita hii imeanza tena.

Kama hayo yote si kweli, basi serikali iyachunguze kwa uwazi.

Lakini kama kuna ukweli ndani yake, basi Watanzania wanapaswa kujua nini kinaendelea nyuma ya pazia.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan tunaomba ulifuatilie jambo hili kwa karibu. Walimu wengi wanaona viongozi waliopo sasa wameleta utulivu mkubwa ndani ya chama na wameanza kurudisha matumaini ya walimu, na hata imani kwa serikali. Kuwaondoa ni kuzua taharuki juu ya maslahi halisi ya serikali na CWT.

Walimu wanalia kimya kimya. Wanajiuliza: kwa nini kila anayesimama kutetea maslahi ya walimu anaonekana kuwekewa vita?

Na kama kweli kuna watu walikuwa wanufaika kwa kiwango cha zaidi ya bilioni moja na nusu kila mwezi kupitia fedha za walimu, basi Watanzania wanastahili kujua ukweli wote.
 
Acha uongo mnajitengenezea ulaji na wewe inaelekea ni mnufaika. Tenda ya kuchspa tshirt na kofia iliuzwa laki tano kwa akili ya kawaida nani anunue tenda kwa laki tano huku haba uhakika wa kushinda. Sio tenda za tshirt hata tenda za venki ya walimu zinatolewa kwa rushwa kubwa.
 
Wazo Zuri
 
Back
Top Bottom