Mimi binafsi sirizishwi na hatua ya serikali sikivu ya CCM kuwakalisha kitaa wahitimu wa vyuo vya ualimu more than 7 months bila sababu za msingi. Hii inaweza kuwaathiri kisaikolojia, kiuchumi na hata kitaaluma. Sioni mantiki ya kufanya hivyo wakati kila siku serikali inawahadaa watanzania kuwa kuna uhaba mkubwa wa walimu!! Kwanini isiwape hata mkataba wa muda wakati wanaweka mambo sawa? Voda fasta wawo mbona walipatikana fasta na fungu likapatikana la kuwalipa? Acheni siasa kwenye elimu jamani.