Walimu waliofunga Shule wakutane Shuleni kwao walau siku moja au mbili kwa Wiki

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736
Habari Wadau,

Kitendo cha Shule za Sekondari na Msingi kufungwa shule kwa ajili ya Corona, kumefanya baadhi ya walimu kuhama maeneo yao ya kazi na kurudi makwao na wengine wako palepale ila wanalewa balaa.

Madeni kibao na matukio mengine ya ajabu. Kuna uwezekano mkubwa baada ya shule kufunguliwa tukapoteza baadhi ya walimu. Wako watakaoacha kurudi shule maana kwa mvua hizi wamejikita kwenye kilimo na kimewalipa, wengine ufugaji lakini wengine wamekuwa walevi na wengine wanadanga!

Ili kuhakikisha walimu wetu wapo au wameshapungua inabidi walau wakutane na mkuu wao wa shule walau mara moja au mbili kwa wiki ili serikali ijiandae mapema. Pia kuna uwezekano wa serikali kuwa inalipa walimu ambao walishaachana na hiyo kazi. Ni hayo tu
 
Complicator......nimeishauri serikali. Faida ni kuwa nina watoto shuleni sitaki wapoteze walimu wao.
Wafundishe mwenyewe! Unashauri ujinga! Hujui kuwa walimu wanasaini payroll kabla ya mshahara wa mwezi husika kulipwa? Usiwe unaanzisha hoja ambazo hazina mashiko!
 
Serikali imesikia. Mnalewa sana
Acha ukuda mtoto wa kiume.nikushauri,wanaolewa lewa nao,wanaodanga wapige miti.
Na kama serikali imewasikia itawachukulia hatua,umewasomesha?.Aya wape hela wamfundishe mwanao home.
Tulia ivo ivo,povu likuishe na ww.walim endeleeni kupiga maji na kudanga mpaka tamko rasmi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe usipende kufatilia Maisha ya wenzako Kuna siku utapigwa miti.
Kila mtu Ana ratiba na plan zake katika dunia hii.
Wewe mienendo yako mibovu Nani anaifatilia?
 
Ta Muganyizi waalimu wamenuia kukupiga miti....chukua tahadhari ikibidi omba ulinzi polisi...Waalimu siyo watu wa mchezomchezo😃😃😃
 
Habari Wadau,

Kitendo cha Shule za Sekondari na Msingi kufungwa shule kwa ajili ya Corona, kumefanya baadhi ya walimu kuhama maeneo yao ya kazi na kurudi makwao na wengine wako palepale ila wanalewa balaa.

Madeni kibao na matukio mengine ya ajabu. Kuna uwezekano mkubwa baada ya shule kufunguliwa tukapoteza baadhi ya walimu. Wako watakaoacha kurudi shule maana kwa mvua hizi wamejikita kwenye kilimo na kimewalipa, wengine ufugaji lakini wengine wamekuwa walevi na wengine wanadanga!

Ili kuhakikisha walimu wetu wapo au wameshapungua inabidi walau wakutane na mkuu wao wa shule walau mara moja au mbili kwa wiki ili serikali ijiandae mapema. Pia kuna uwezekano wa serikali kuwa inalipa walimu ambao walishaachana na hiyo kazi. Ni hayo tu
Wanalewa pesa Yao na hawali wala kulala kwako,,,Wakiacha kazi serikali itaajiri walimu wengine,,,KUNA KA WIVU NAKAONA PAHALI #WANADANGA BALAA#
 
Back
Top Bottom