Walimu wanajidhalilisha kutokana na yafuatayo:

Walimu wanajidhalilisha kutokana na yafuatayo:

Katika uchunguzi wangu nimebaini mshahara wa Kanda ya ualimu kibongo bongo ni mkubwa kiukweli ila nikabaini mambo yafuatayo ndio yanaifanya Kanda hiyo kudharaulika katika jamii...

1.Mavazi hasa walimu wa kiume wanavaa suluari Pana za kijivu na mashati mekundu.

2.Viatu vyenyewe four angle

3.Majungu, mwalimu yupo radhi amchongee mwenzake Kwa mkuu wa shule ili yeye apate fursa zipatikanazo mara moja Kwa mwaka za usimamizi.

4.Hawana posho Wala marupurupu lakini wameamua kuridhika tu na kuwaza kujiendeleza kimasomo ili wapate degree na masters huku familia zikiteseka.Wengi hawawazi mbinu mbadala za kupata pesa

Kwa watu wenye focus hii kazi ni nzuri sana hasa serikalini maana Wana muda mwingi sana wa kuweza kusimamia mambo mengine.
Mshahara mkubwa unaanzia Bei gani?
 
Hawana posho Wala marupurupu,wewe umejuaje? Au wewe pia ni mwalimu?
Kwa kifupi ni kuwa, ukiona mtu anaponda sana walimu au taaluma flani, ujue na yeye ni mmoja wao au alikuwa mmoja wao.

Mfano, huyu mtoa mda ni mwalimu au alikuwa mwalimu akaacha kwa either kufukuzwa au kupata kazi nyingine (probably recategorisation) na wakati akiwa mwalimu aliwahi kuonewa onewa, hivyo ni kama amejenga nao chuki.

Kwa mtu ambaye akili zake ziko sawa sawa hawezi kushinda kutwa kucha anaongelea maisha ya walimu ambao kila siku wanakaa na watoto wake kwa zaidi ya masaa 9
 
Mshahara mkubwa unaanzia Bei gani?
Laki 7/8/9 kwa walimu wa Serekali (sio private) huo ndio mshahara mkubwa, ingawa kuna Mwalimu wa primary yeye na mkewe wote walimu wamepanga nyumba nzima, watoto wao wanasoma kwenye magari ya njano sio kayumba na wanafundisha shule za Serekali yaan primary sasa jiulize wanalipwa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom