Walimu wanamsingizia kiuonevu mwanangu, je ni hatua gani nichukue kama mzazi?

Walimu wanamsingizia kiuonevu mwanangu, je ni hatua gani nichukue kama mzazi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Ipo hivi, mwanangu anasoma shule fulani English medium, mimi haya mambo ya schoolbus niliyakataa kabisa maana kuna wenzake wengi tu wanatembea na hata mimi baba yake siijui school bus maisha yangu ya elimu, ila pia niliona atembee tu ili kunyoosha miguu kwa afya yake.

Sasa pale shuleni kwao yeye yupo na wenzake wachache sana wenye utaratibu kama wake, yeye na wenzake wasiopanda schoolbus ama kufatwa na usafiri binafsi wakitoka shule huwa wanacheza mpira kiwanja cha shule fulani ya karibu na wenzao wa shule nyingine, watapiga piga stori njiani na michezo michezo mingine maana naona saizi anapenda kuruka sarakasi itakuwa labda alifundishwa huko huko.

Sasa naona huenda wenzake walikuwa hawapendi hii kitu, baadhi wakaanza kuwaambia wazazi wao kwamba wanaweza kwenda na kurudi kutoka shule bila school bus au usafiri binafsi kwa hiyo nao waanze kurudi nyumbani kivyao

Sasa baada ya hii ishu kwenda sana ndio baadhi ya wazazi wakafika shuleni na baada ya kuchuimbua chimbua ndio wakafikia hatua kudai mwanangu na marafiki zake wachache wanaoendaga nyumbani bila msaada ndio wanawatia sumu watoto wao.

Mwanangu nimeongea nae, yeye kasema hajashawishi yeyote kuacha kupanda schoolbus,

Sasa hapa binafsi kama mzazi naona mwanangu hana kosa na inabidi watengue hii kauli, nimepewa barua nifike Ijumaa
 
Jifunze hili; Mtoto huwa hawezi kuchuja maneno kama mtu mzima. Haelewi yapi aseme na yapi asiseme.

Inavyoonekana wewe huwa unaongea vitu mbele ya mwanao bila kuchuja, hujatambua kwamba anachosikia mwanao kutoka kwako, anaenda kukipeleka vivyo hivyo shuleni na hata kwa mwalimu.

Anza kupima maneno gani useme mbele ya mtoto na yapi sio ya kusema, la sivyo atafikisha maneno yako jinsi yalivyo.
 
Shule nyingi zipo kibiashara, hapo ni kwamba waalimu wameona wanakosa wateja wa watoto wanaoenda na school bus,hivi mpaka shuleni haifiki kilomita 1 halafu school bus tena?au unapokaa mzazi Hadi shuleni haifiki kilomita moja halafu walazimishe mtoto akae bweni?
 
Shule nyingi zipo kibiashara ,hapo ni kwamba waalimu wameona wanakosa wateja wa watoto wanaoenda na school bus,hivi mpaka shuleni haifiki kilomita 1 halafu school bus tena?au unapokaa mzazi Hadi shuleni haifiki kilomita moja halafu walazimishe mtoto akae bweni?
Kweli mkuu
 
Ipo hivi, mwanangu anasoma shule fulani English medium, mimi haya mambo ya schoolbus niliyakataa kabisa maana kuna wenzake wengi tu wanatembea na hata mimi baba yake siijui school bus maisha yangu ya elimu, ila pia niliona atembee tu ili kunyoosha miguu kwa afya yake...
Niuzie Mimi hiyo kesi tufanye huyo ni mwanangu
 
Nilichokiona hapo ni hao watoto wengine hawataki kupanda basi la shule ili wapate muda wacheze mpira (na ukifanyika uchunguzi wengi wanaokataa kupanda mabasi ni wavulana)kawaida watoto wanapenda michezo na zile stori za mpira waliocheza wenzao zinawavutia na wao kutamani kucheza.

Pia nyumbani kwao inawezekana wanabanwa sana hawana muda wa kutosha kucheza,kuchanganyika na watoto wenzao nk.
 
Back
Top Bottom