JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi nchini, linawashikilia walimu 4 na mfanyabiashara mmoja, kwa tuhuma za kuwatapeli wananchi kwa kuwadanganya kuwekeza katika sarafu za kimtandao (cryptocurrency) na matokeo yake kutoweka na fedha zao walizowekeza.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime, wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo, alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika Hotel ya Gold Crest, Jijini Mwanza, mara baada ya kupokea malalamiko ya wananachi kutapeliwa fedha zao.
Amesema hivi karibuni kumeendelea kujitokeza tabia za baadhi ya watu kutapeli watu wengine, kwa kuwalaghai kuwa wao ni wawekezaji wa sarafu ya mitandaoni, ambapo matapeli hao ili kukamilisha utapeli wao wamekuwa wakifungua mifumo na makampuni, ambayo baadhi wameyapa majina ya Meme Bank, Digital Wealth International, Octoquant AI Trading, Npama Fund, Mindful Trade na Celestrial TG Cryptocurrency.
Chanzo: ITV