Walimu waongoza kwa kuolewa ukilinganisha na sekta nyingine

Walimu waongoza kwa kuolewa ukilinganisha na sekta nyingine

yap wanamsomo ya kimaadili pia kazi zao huwapa muda wa kuwa na familia wana malezi mema kutokana na taaluma si rahisi kukuta mwalimu anafanya uchafu hadhrani kama kunywa pombe sana ama ngono, wanavaa kiheshima so soko liko juu
 
Ngoja na mimi nihamie kwenye fani ya ualimu:msela:
 
Je walimu wa kike wa chuo nao wanafaa? Naomba mnijuze wadau!
 
kwa hiyo walimu ndio wanaoolewa kwa sana tu, mbona hata bank ukieda kila teller nae anapete yake? au inakuaje na hili
 
Je walimu wa kike wa chuo nao wanafaa? Naomba mnijuze wadau!

Sina uzoefu wa vyuo vingine lakini ukienda udsm ukikutana na msichana anayesoma education utamjua tu bila hata kumuuliza anasoma kozi gani kulingana na anavyoonekana tu kwa nje na mavazi yake, sio rahisi kumkuta kavaa vipedo, suruali wala vinguo vya ajabu kama wanavyovaa mademu wa Sociology, Bcom au kozi nyingine.

Pia walimu wa Education wengi ni wakali sana kwenye maadili, nakumbuka kuna mama mmoja ni Prof. wa education na (sina uhakika kwa sasa) alikuwa dean wa kitivo cha elimu main campus alikuwa akipita kwenye vipindi mbalimbali kukagua mavazi ya wanafunzi na akimkuta mtu kavaa vibaya anamtoa lecture. Hata wanaume hawakuwa wanaruhusiwa kuvaa jeans au kuvaa shati bila kuchomekea
 
  • Thanks
Reactions: SG8
kwa hiyo walimu ndio wanaoolewa kwa sana tu, mbona hata bank ukieda kila teller nae anapete yake? au inakuaje na hili

Pete lazima wawenazo si unajua wasanii wengi!!! ila mke wa kweli ni mwalimu, nesi anafuatia na wengine vilaza
 
Wanasheria hata wanaume ni hovyo. Si good partners. Nina kaka yangu mbishi huyo yani akiwa nyumbani hakuna kupiga story maana anapenda cross examination utasema tuko mahakamani. Kila kitu anataka evidence.

Owa mwanasheria uone moto wake!
 
wanalikizo mara mbili kwa mwaka ambayo ni tofauti na likizo yake ya kawaida<br />
hawaingii kazini siku za jumamosi na jumapili ukilinganisha na manesi/bankers<br />
wanakuwa na fikra endelevu.
<br />
<br />
Si kweli kuwa Mwl ana likizo nyingine ya kawaida mbali na hizo mbili kubwa za wanafunzi. Kwa mujibu wa Teachers' Service Scheme ya mwaka 2008, Mwalimu anaruhusiwa kuchukua likizo ya mwaka ambayo ni 28days wanafunzi wanapokuwa likizo ndefu i.e Juni au Desemba kwa wale wa darasa la kwanza mpaka form four. Hivyo basi kiuhalisia na kwa mujibu wa Scheme hyo likizo ya pili hatakiwi kuwa mbali na mazingira ya kazi, anaweza kuhitajika kuwepo kazini kwa kazi nyingine.
Back 2the point, ni kweli mwalimu mwanamke ni mke bora kwani ni walezi wazuri wa familia hasa wale wa Primary Education.
 
Kusema ukweli mimi si mwalimu ila kweli walimu wazuri, as long as una kipato cha kutosha nashauri uoe mwalimu wana muda na wanajua saikolojia ya kulea watoto. Tatizo kama kipato chako kama changu maisha yatakuwa magumu ukioa teacher.
 
Japokuwa walimu ni wake wazuri haina maana sisi wengine hatuna soko; ndio maana tumeolewa ila wame zetu cha moto wanakiona!
 
True, wanaume wazembe hukimbilia wanawake kama walimu ili wawaonee vizuri. Mie binafsi naona walimu hawana changamoto kwanza wanaboa, they r too overdecent.
Labda tu wewe mwenzetu mwenye akili nyingi na maarifa ya hali ya juu ungetusaidia tu kutueleza mpaka hapo ulipofikia ukawadharau walimu, je wewe umefundishwa na nani?
Ficha upumbavu wako na usifiche hekima yako.
 
hii thread inakoelekea kubaya... Je na walimu wa kiume JE!?
 
Mhhhh kwa hiyo wengine hapa ni galasha tu au?
 
Wanaume wengi hawapendi wanawake wenye vipato vya juu. Hivyo mostly walimu ndo wanyonge wao, lol
Hii inawezekana ina ukweli lakini hata hivyo mara nyingi tatizo huwa sio kipato ila ni ile tabia inayoletwa na uwepo wa kipato kikubwa kwa mwanamke kuliko mwanaume. Hii tumeshajadili hapa, kuwa mara nyingi kwenye ndoa mwanamke akiwa na kipato kikubwa kuliko mwanaume hali huwa tete sana. Najua kuna watu watabisha lakini ni ukweli usiopingika kuwa fedha ina tabia ya kubadilisha watu japo si wote.

Pili kuna kazi nyingine zina mazingira hatarishi sana. Fikiria msichana anayefanya kazi benki anakutana na vishawishi kiasi gani?! Japokuwa ni kweli kuwa suala la kushawishika kwa mtu kunategemea na msimamo wa mtu lakini pia ni kweli kuwa kadri vishawishi vinavyozidi ndivyo chansi ya kuangukia katika dhambi inapokuwa kubwa.

ngoja niishie hapa kwanza nitarudi.
 
Back
Top Bottom