Mjamaa masalia
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 373
- 354
Kumekuwa na shauku kubwa sana ya Walimu kupangiwa vituo vya kazi na serikali na hii imetokana na danadana za serikali yetu kutoa taarifa za kujikanganya mara kwa mara. Kwani imefikia hatua kila mwezi una tamko lake la ajira toka kwa waziri tofauti
Lakini labda habari ya hivi karibuni inaweza ikawa na ukweli kwamba mwezi wa nne tarahe mosi ndio siku ya kuripoti, ikiwa ni kweli
JE WALIMU MMEJIANDAAJE KWENDA KURIPOTI?
Ieleweke wazi kuwa hapa nazungumzia maandalizi ya aina mbili,
NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA
===========================
===========================
Lakini labda habari ya hivi karibuni inaweza ikawa na ukweli kwamba mwezi wa nne tarahe mosi ndio siku ya kuripoti, ikiwa ni kweli
JE WALIMU MMEJIANDAAJE KWENDA KURIPOTI?
Ieleweke wazi kuwa hapa nazungumzia maandalizi ya aina mbili,
- kwanza ni maandalizi ya kisaikolojia, inawezekana mtu amejipangia kuwa yeye atapangiwa mjini, je ikitokea umepanga kijijini, umejiandaaje kisaikolojia? hapo bila kujiandaa kisaikolojia utakuwa na wakati mgumu sana kwa kweli nina amini utaichukia na kazi kwani utakuwa unaifanya kwa majuto makubwa sana.
- .MAANDALIZI YA KIFEDHA
hapa pana umuhimu mkubwa sana kwani nina imani kuwa wengi watapangiwa sehemu tofauti na mahali wanapoishi kwa sasa, nikiwa na maana mkoa mwingine hivyo kuna maandalizi ya pesa ya kujikimu kwa wakati utakapo kuwa huko, kwani nin nadra sana pesa ya serikali kutoka mapema
USHAURI
USHAURI
- Jiandae na pesa ya kukaa guest walau wiki moja unavyofuatilia mchakato wa kuripoti na kupangiwa kituo(Shule) pia chukua tahadhari kuna maeneo hayana hizo nyumba za kulala wageni.
- Jiandae na pesa ya kupanga chumba walau kwa miezi 6, kwanza, hiyo itasaidia kupunguza gharama za kulala Nyumba za wageni wakati pesa yako ya kujikimu na ya mshahara haijatota
- Jiandae kwa pesa ya godoro kwanza( kama una uwezo wa kununua na kitanda basi hewala} lakini walau ukiwa na godoro utapata usingizi
- Hivyo nashauri ni bora ukawa na pesa binafsin ya kujikimu, ili uweze kumudu gharama za chakula pamoja na mambo mengine, kuliko kuitegemea sana hiyo pesa ya serikali ambapo urasimu ni mwingi,
NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA
===========================
===========================
Utakapoliona jina lako na sehemu ulipangiwa, hakikisha kwamba:
1) Ndani ya siku 3 tayari umeshafungasha virago vyako kuelekea ulipopangiwa- hii itakusaidia kwenda kuyajua mazingira yako ya kituo cha kazi na jinsi utakavyopambana na changamoto za chaka.
2) Hakikisha umebeba vyeti halisi na wala sio photocopy- hii itakusaidia kuondoa usumbufu wa kukuingiza kwenye system ya mshahara maana nilishawaonaga walimu wengi pale baraza la mitihani (NECTA), wakiwa wanahangaika wakati wenzao wapo vituo vya kazi.
3) Hakikisha angalau una kianzio(pesa) ya kujikimu angalau ya siku 2 kuepuka usumbufu unaoweza kutokea halmashauri zenu- kuna walimu nilishawaonaga walienda kuomba kulala kwa mwenyekiti wa kijiji... Nasisitiza hasa kwa wadada mana hii huwaga ni advantage ya watu wengine kutaka kuwarubuni wadada walimu ili watoe papch.
4) Kwa wale wajasiriamali (entrepreneur) hakikisha unayasoma mazingira vizuri ili usije ukategemea mshahara pekee- nimewahi kuwaona walimu wakilalamika tarehe za mwanzo kuwa mshahara umekata.
5) Fanya kazi kwa bidii kuleta tija katika hili taifa kwa kuwa ualimu ni sawa na mapigo ya moyo ya taifa.
6) Achaneni na mambo ya mikopo wakati ndio kwanza hata mwaka hujamaliza sjui sacos, vicoba au hata mabenk makubwa. Nimewahi kuona walimu wakilia sana jamaa walikuja kusafisha chumba.
7) Chagueni mifuko ya kibima yenye makato nafuu, hapa unatakiwa uwe makini sana bila kukurupuka.
8) Changamoto ni nyingi sana ila naimani mlifundishwa vyuoni jinsi ya kukabiliana nazo, hii sio kwenye ualimu pekee bali kwenye kada zote.
9) Kujifunza kusave mshahara ni kitu muhimu sana ili kufikia malengo uliyojiwekea itashangaza kuona mwalimu umefanya kazi mwaka mzima bila kuwa na mradi wa nyongeza.
10) MWISHO NAWATAKIA WALIMU WOTE TARAJALI HERI NA MAFANIKIO MEMA KUELEKEA AJIRA MPYA.