Walimu wapya mmejiandaaje kuripoti vituo mtakavyopangiwa?

Walimu wapya mmejiandaaje kuripoti vituo mtakavyopangiwa?

Mjamaa masalia

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2012
Posts
373
Reaction score
354
Kumekuwa na shauku kubwa sana ya Walimu kupangiwa vituo vya kazi na serikali na hii imetokana na danadana za serikali yetu kutoa taarifa za kujikanganya mara kwa mara. Kwani imefikia hatua kila mwezi una tamko lake la ajira toka kwa waziri tofauti

Lakini labda habari ya hivi karibuni inaweza ikawa na ukweli kwamba mwezi wa nne tarahe mosi ndio siku ya kuripoti, ikiwa ni kweli

JE WALIMU MMEJIANDAAJE KWENDA KURIPOTI?

Ieleweke wazi kuwa hapa nazungumzia maandalizi ya aina mbili,

  • kwanza ni maandalizi ya kisaikolojia, inawezekana mtu amejipangia kuwa yeye atapangiwa mjini, je ikitokea umepanga kijijini, umejiandaaje kisaikolojia? hapo bila kujiandaa kisaikolojia utakuwa na wakati mgumu sana kwa kweli nina amini utaichukia na kazi kwani utakuwa unaifanya kwa majuto makubwa sana.

  • .MAANDALIZI YA KIFEDHA
hapa pana umuhimu mkubwa sana kwani nina imani kuwa wengi watapangiwa sehemu tofauti na mahali wanapoishi kwa sasa, nikiwa na maana mkoa mwingine hivyo kuna maandalizi ya pesa ya kujikimu kwa wakati utakapo kuwa huko, kwani nin nadra sana pesa ya serikali kutoka mapema
USHAURI

  1. Jiandae na pesa ya kukaa guest walau wiki moja unavyofuatilia mchakato wa kuripoti na kupangiwa kituo(Shule) pia chukua tahadhari kuna maeneo hayana hizo nyumba za kulala wageni.
  2. Jiandae na pesa ya kupanga chumba walau kwa miezi 6, kwanza, hiyo itasaidia kupunguza gharama za kulala Nyumba za wageni wakati pesa yako ya kujikimu na ya mshahara haijatota
  3. Jiandae kwa pesa ya godoro kwanza( kama una uwezo wa kununua na kitanda basi hewala} lakini walau ukiwa na godoro utapata usingizi
  4. Hivyo nashauri ni bora ukawa na pesa binafsin ya kujikimu, ili uweze kumudu gharama za chakula pamoja na mambo mengine, kuliko kuitegemea sana hiyo pesa ya serikali ambapo urasimu ni mwingi,
Hivyo kipindi hiki mnacho subiri post basi sio vibaya kufanya shughuli ndogondogo za kukupa kipato walau upunguze mahitaji madogomadogo wakati wa kuripoti

NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA

===========================
===========================


Utakapoliona jina lako na sehemu ulipangiwa, hakikisha kwamba:

1) Ndani ya siku 3 tayari umeshafungasha virago vyako kuelekea ulipopangiwa- hii itakusaidia kwenda kuyajua mazingira yako ya kituo cha kazi na jinsi utakavyopambana na changamoto za chaka.

2) Hakikisha umebeba vyeti halisi na wala sio photocopy- hii itakusaidia kuondoa usumbufu wa kukuingiza kwenye system ya mshahara maana nilishawaonaga walimu wengi pale baraza la mitihani (NECTA), wakiwa wanahangaika wakati wenzao wapo vituo vya kazi.

3) Hakikisha angalau una kianzio(pesa) ya kujikimu angalau ya siku 2 kuepuka usumbufu unaoweza kutokea halmashauri zenu- kuna walimu nilishawaonaga walienda kuomba kulala kwa mwenyekiti wa kijiji... Nasisitiza hasa kwa wadada mana hii huwaga ni advantage ya watu wengine kutaka kuwarubuni wadada walimu ili watoe papch.

4) Kwa wale wajasiriamali (entrepreneur) hakikisha unayasoma mazingira vizuri ili usije ukategemea mshahara pekee- nimewahi kuwaona walimu wakilalamika tarehe za mwanzo kuwa mshahara umekata.

5) Fanya kazi kwa bidii kuleta tija katika hili taifa kwa kuwa ualimu ni sawa na mapigo ya moyo ya taifa.

6) Achaneni na mambo ya mikopo wakati ndio kwanza hata mwaka hujamaliza sjui sacos, vicoba au hata mabenk makubwa. Nimewahi kuona walimu wakilia sana jamaa walikuja kusafisha chumba.

7) Chagueni mifuko ya kibima yenye makato nafuu, hapa unatakiwa uwe makini sana bila kukurupuka.

8) Changamoto ni nyingi sana ila naimani mlifundishwa vyuoni jinsi ya kukabiliana nazo, hii sio kwenye ualimu pekee bali kwenye kada zote.

9) Kujifunza kusave mshahara ni kitu muhimu sana ili kufikia malengo uliyojiwekea itashangaza kuona mwalimu umefanya kazi mwaka mzima bila kuwa na mradi wa nyongeza.

10) MWISHO NAWATAKIA WALIMU WOTE TARAJALI HERI NA MAFANIKIO MEMA KUELEKEA AJIRA MPYA.


 
kwel ila hao wenyew wamezungumza kwamba safar hii itakuwa n tofauti yaan huo mwez unaoenda kuripoti basi mwisho wa mwez wake unaanza kuchukua mshahara
 
Ni vizuri kuchukua tahadhari kwani tatizo viongozi wetu kila jambo wanatanguliza siasa kwanza kabla ya utendaji,wakifanya hivyo watakuwa wamewasaidia wengi sana
 
Nauona mwezi huu ukiingia katikati,ngoja tutaona!
 
Usiwatishe serikali sikivu ya chama tawala imejipanga kuwapokea walimu kwenye vituo vyao vya kazi watakapo pelekwa. Itawalipa stahiki zao kama utaratibu unavyo elekeza. Walimu wakafanyekazi,wasikimbie vituo kwa majungu ya baadhi ya watu na wanasiasa.
 
Usiwatishe serikali sikivu ya chama tawala imejipanga kuwapokea walimu kwenye vituo vyao vya kazi watakapo pelekwa. Itawalipa stahiki zao kama utaratibu unavyo elekeza. Walimu wakafanyekazi,wasikimbie vituo kwa majungu ya baadhi ya watu na wanasiasa.

Sasa mkuu mimi siwatishi najaribu kutoa tahadhari kwa uelewa wangu mdogo,hata kama watatoa hizo stahiki zao kwa wakati pia lazima tujiulize je zitakidhi mahitaji ya msingi ya mwanzo mfano: pango la nyumba(kama shule haina nyumba za walimu),hiyo pesa itatosha kununua kitanda,godoro,kulipa guest siku za mwanzo?

Hahaha ila yote yanawezekana kupitia serikali sikivu, kuna walimu wataambiwa mtalala kwa mkuu wa shule mpaka mtakapo pata nyumba
 
Acha kujiradharau kaka,wewe huna uelewa mdogo.
Mambo uliyoyadokeza hapo ni ya msingi sana!

Nimekupata mkuu, sema nimeona mdau kaja na hoja kwamba mimi na watishia walimu wapya, wakati mimi nilikuwa natoa angalizo, hasa maandalizi ya kisaikolojia ni muhimu sana, na watu wengi wambao wamekuwa wakiilalamikia taaluma hii ni kwa sababu ya kukosa maandalizi ya kusoma ualimu wenyewe pamoja na kufanya kazi yenyewe.
Tupo pamoja mkuu, ahsante kwa credit
 
Daa''kwanza siamini kama april mos walimu watapata vituo vipya'hii imetokana na serikali kupitia wizara husika kutotoa tamko rasmi kuhusu ajira mpya.Hivyo wahitimu walio wengi naamini hawajajipanga vema kuungia kazni kwani serikali ni sumbufu juu ya swala hilo
 
Lets wait and see, ukisha pata kazi mambo mengine yote yatajipanga tu yatake yasitake.
 
Kitu unachokisubiria kwa hamu sana kinaongezeka value.

Ndo maana serikali yenu imeamua kuwasubirisha kwa mda. Usipate hofu ifikapo april ukaambiwa endelea kusubiri. Waalimu wenzangu la msingi ni kujipanga kama mtoa mada anavyo kutaka. Usiishie kulala na kulalamika. Nahc ukiwa na milioni moja itakutosha kuanzia maisha. Hapa kenya mwalimu kuajiriwa ni wewe ukaombe na sio Government ikupange. Tumia mda huu kwa usahii. Wenye wachumba hakikisha umefanya ndoa.

Wenye hawana wang'ang'ane ndo mda.
 
Asante Kwa Ushauri Bro Pia Inatakiwa Kuwa Makin Ktk Ufuatiliaji Wa Hizo Pesa Kwa Mfano Nauli Vinginevyo Unaweza Kuzurumika Mana Wajanja Ni Wengi! Nawatakieni Maandalizi Mema, Ualimu Ni Kazi Rahc Ila Kuna Baadh Ya Walimu Wanacomplicate Mpaka Tunaona Ni Mgumu.
 
kwel ila hao wenyew wamezungumza kwamba safar hii itakuwa n tofauti yaan huo mwez unaoenda kuripoti basi mwisho wa mwez wake unaanza kuchukua mshahara
viongozi wetu ni wepesi sana kusema kuliko kutenda, mtoa mada amewapa tahadhari nzuri
 
Back
Top Bottom