Haludzedzele
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,468
- 530
Walidhan kupata ajira ndo mwisho wa matatizo? Na huu ni mwanzo tu wataexperience meengi saana hii ndo kada ya kinoko kazi ipo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanadharau waalimu halafu matokeo yakija mabaya wanaunda tume.
Hilo ni suala la kawaida kwenye utumishi wa umma mi mbona nilikaa miezi 9 na badae nililipwa na malimbikizo yote ya mishahara yangu,watanzania wanapenda sana kulalamika.
HAYA NDO MAFISADI YENYEWE! JITU LINAONGEA TU BILA HATA YA KUFIKIRI! kwa hiyo na hawa unataka wakae miezi tisa bila mishahara? Kuna kipindi huwa nnahofu san na akil zetu watanzania!! Unaweza kumpeleka mwanao shule bila ada na akirudishwa nyumban utahoji kwamba anaonewa kwa sababu wewe ulisoma bila kulipa ada!
mkuu,umepitia kwa makini sheria ya ajira/kazi ya tanzania?? Ujira/malipo ni haki ya msingi ya mtu na ilipwe kwa wakati stahiki (kwa mujibu wa mkataba). Katika hali kama hiyo,neno "wanapenda kulalamika" halina mashiko. Kama ulilipwa baada ya miezi 9,unataka kutuaminisha kuwa ulistahili malipo yako yalipwe kwa muda huo?? Wale ambao hawalipwi kwa muda "wakizungumza" ndiyo kulalamika?? Unataka kuwaaminisha wote wanaodai haki zao za malipo "wasilalamike",waendelee kufundisha?? Vipi kuhusu mahitaji yao ya msingi yanayotegemea "mshahara na masurufu" yatokayo na ajira yao ya ualimu?? Nayo yasubiri miezi 9 kama yako?? Umeamua kuitetea serikali,jenga hoja za msingi..
Asante ndugu, haya si ndio yale majitu yasiyojua haki zao za msingi!!! Bora linyamaze kama kichwani ni KINDERGATEN
Toka Wilaya ipi sasa? Ninachojua mimi Walimu waliajiriwa tarehe 1/3/2013 na sio mwisho wa mwezi wa piliWalimu wapya walionza kazi mwishoni mwa mwezi wa pili wameanza kutaabika baada ya kukuta hamna majina yao kwenye Payrol ,huku wakurugenzi Wakiwakwepa kuwasaidi,habari nilizopata kutoka Wilayani zinasema mkurugenzi kawatolea nje kuwasaidia!Mwanzo wa malimbikizo na mizozo ndio huanzia hapa.
Toka Wilaya ipi sasa? Ninachojua mimi Walimu waliajiriwa tarehe 1/3/2013 na sio mwisho wa mwezi wa pili
Walidhan kupata ajira ndo mwisho wa matatizo? Na huu ni mwanzo tu wataexperience meengi saana hii ndo kada ya kinoko kazi ipo
Hapa ndipo ugumu wa maisha ya ualimu unapoanzia,hao walimu wataanza kukopakopa ili wajikimu kimaisha,mwisho wake ni kuwa na madeni lukuki miezi michache tu baada ya kuanza kazi.Hii ndiyo TZ ya Watanzania.