Huwezi amini mpaka sasa walimu wapya katika Halmashauri ya Bumbuli hawajalipwa pesa yao ya kujikimu, nauli wala mshahara na wanaambiwa mshahara haukupatikana kwa vile serikali haina pesa,kwa hiyo tutegemee labda mwezi wa tano au wa sita. Sasa walimu wapya ili waishi inabidi wawe omba omba, haya ndio maisha halisi ya huku Bumbuli. Hii ni sehemu ambayo maisha ni magumu mno tofauti na mikoa kama vile Mbeya, Songea, Usafiri huku ni wa bodaboda na wa gharama sana. kwa kweli utajuta kuwa mwalimu katika Halmashauri hii, ni maisha mabovu mno, hamna pesa na watendaji wake hawajali wala kuwahurumia walimu wake, kila mtu na mambo yake ya kumletea maendeleo yake binafsi.