Walimu watatu washikiliwa na TAKUKURU Kagera kwa udanganyifu

Walimu watatu washikiliwa na TAKUKURU Kagera kwa udanganyifu

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera tumeendelea kutekeleza majukumu yetu kama yalivyoainishwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007. Katika utekelezaji wa majukumu yetu tumeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya Rushwa wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla. Aidha majukumu haya yametekelezwa katika wilaya zote zilizo chini ya Mkoa wa Kagera.

Ndugu waandishi wa habari,

Tunapenda kuujulisha umma kuwa tunawashikilia waalimu watatu wa Shule ya Sekondari Kalenge (Kalenge Day) iliyoko Kata ya Kalenge Wilayani Biharamulo kwa tuhuma za Matumizi mabaya ya ofisi chini ya kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 na kufanya usajili kwa udanganyifu chini ya kifungu cha 309 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 (Kama ilivyorekebishwa mwaka 2002)

Ndugu wanahabari,


Waalimu wanaoshikiliwa ni wafuatao:
  • Mwl. BONIPHACE ELIAB ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kalenge (Kalenge Day ),
  • Mwl EDWIN VALENTINE ambaye ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kalenge ( Kalenge Day) na
  • Mwl GREVAS RICHARD ambaye ni Mwl wa Taaluma Shule ya Sekondari Kalenge (Kalenge Day).
Ndugu wanahabari,

Walimu tajwa wanashikiliwa kufuatia kupokelewa kwa taarifa mnamo tarehe 19/06/2020 iliyokuwa ikiwatuhumu waalimu hao kwa tuhuma za kufanya udanganyifu wakati wa mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana (2019).

Uchunguzi wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera ulibaini kwamba Walimu hawa walimfukuza shule mwanafunzi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kisingizo cha kuwa alikuwa mgonjwa na kisha wakati wa kufanya mitihani ulipofika, kwa njia za RUSHWA waliitumia namba ya mwanafunzi huyo aliyefukuzwa ya mtihani na kumpatia mwanafunzi mwingine ambaye aliufanya mtihani huo.

Ndugu wanahabari,


Uchunguzi wetu umebaini pia kuwa, mara baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka, Jina la mwanafunzi aliyekuwa amefukuzwa lilionekana kuwa amefaulu kwa kupata daraja la pili (Division two) huku ikiwa inafahamika kuwa mwanafunzi halisi mwenye jina hilo alishafukuzwa na hakufanya mitihani.

Hali hii ilimfanya mzazi wa mwanafunzi aliyekuwa amefukuzwa shule kushikwa na mshangao na hivyo kuamua kutoa taarifa TAKUKURU.

Ndugu wanahabari,

Uchunguzi wa TAKUKURU umeweza kubaini pia kuwa katika Shule ya Sekondari Kalenge (Kalenge Day) mwaka jana (2019) mwezi wa nane kuna mwanafunzi ambaye alikuwa akiumwa macho na wakati anaendelea na matibabu viongozi wa shule tajwa walimtaarifu kuwa amefukuzwa shule kwa utoro na hivyo mwanafunzi huyo hakuweza kuendelea tena na shule.

Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, uchunguzi wetu umebaini pia kuwa wakati mwanafunzi huyo mgonjwa wa macho ametaarifiwa juu ya kufukuzwa kwake shule, uongozi wa shule hiyo kwa njia za RUSHWA ulimwingiza mwanafunzi mwingine ambaye jina lake limehifadhiwa na kwamba wakati wa mitihani mwanafunzi huyo alifanya mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya sekondari kwa kutumia namba na majina ya mwanafunzi aliyedaiwa kufukuzwa na kwamba matokeo ya kidato cha nne yalipotoka yalionyesha jina na namba ya mwanafunzi aliyedaiwa kufukuzwa kwamba amefaulu kwa kipata daraja la pili (DIVISION TWO) huku mwanafunzi halisi akiwa hakufanya mtihani wowote.

Kutokana na matukio hayo yote, TAKUKURU iliamua kuwashikilia waalimu hawa wote kwa mahojiano zaidi.

WITO:

Tunatoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Kagera kuendelea kushirikiana na TAKUKURU na Serikali kwa ujumla katika mapambano dhidhi ya Rushwa kwani Rushwa husababisha uvunjifu wa haki za binadamu. Humong’onyoa imani ya Wananchi kwa Serikali yao na hudhoofisha maendeleo.

Ikumbukwe kuwa tunaweza kuwa na maendeleo endelevu iwapo HAKI itatawala miongoni mwetu kwa kuwa HAKI inainua Taifa lenye watu wenye AMANI na FURAHA. Pia tumebainisha kuwa RUSHWA inaondoa HAKI, na HAKI ikiondoka AMANI na FURAHA vitapotea. AMANI na FURAHA vikipotea hakuna MAENDELEO yoyote yatakayopatikana kwa Taifa na kwa mtu binafsi.
 

Attachments

Wanafanya mchezo wakijinga hivyo, kama hawajasoma! hizo dili watuachie sisi! wakanye debe lakujitakia sasa
 
Kuna shule nyingine qt na risitaz wanasoma pamoja darasani. Nitakinukisha muda sio mrefu
 
Hawa jamaa inatakiwa wamlipe fidia dogo maana wamemuharibia future yake ili iwe fundisho kwa wengine
 
MATOKEO ya mitihani yote yawe yanaandikwa na majina urudishwe utaratibu wa zamani hili la kutoa namba ya mwanafunzi na matokeo bila jina watu waovu watacheza sana michezo kama ya hiyo shule na inawezekana ilishachezwa sana
 
Wasisahau pia kumkamata na msimamizi wa huo mtihani maana kabla ya hao wanafunzi kuanza kufanya hiyo mitihani yao ya Taifa, wanatakiwa kuthibitishwa kama ndiyo wenyewe! kupitia picha zao maalum (Photo Entry) zilizotumwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Duh!!! Kuna mlolongo hapaa
.
 
Wakati mwengine inakuaga ni roho mbaya tu ya wazazi unakuta mtoto wao aliacha shule zamani inafika kipindi Cha mtiani ndo wanampeleka au wamesikia jina lake linatumika na mtu wanaanza vurumai ilihali wote wakose
 
Wakushikwa hapo sio hao walimu tu ,wasisahaulike wasimamizi wote maana hilo dili haliwezi kuwa la msimamizi wa mkondo huo huo mmoja
 
Back
Top Bottom