Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Walimu watelekeza shule, watimkia mgodini
na Sitta Tumma, Mwanza
WALIMU wa Shule ya Msingi Nyakunguru B iliyopo katika Kijiji cha Nyakunguru, Kata ya Kibasuka, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, wametelekeza kazi yao na kutimkia katika mgodi wa dhahabu wa Itandura kwa ajili ya kuchimba madini.
Wanadaiwa kukimbilia mgodini hapo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni maisha magumu, hali ambayo imewafanya muda mwingi washindwe kufundisha ipasavyo.
Vyanzo vya habari kutoka mgodini hapo vimeieleza Tanzania Daima kuwa, walimu hao wamekuwa wakifika mgodini nyakati tofauti, huku baadhi yao wakiapa kutoendelea na kazi yao ya kufundisha wanafunzi shuleni.
Kwa mujibu wa habari hizo, shule hiyo inadaiwa kuwa na walimu wanne, lakini wote wamekacha kazi hiyo na kujiunga na wachimbaji wadogo na kuwaacha wanafunzi wakishinda madarasani bila kufundishwa.
Mimi namiliki mashimo kwenye mgodi huu wa Itandura na ninapozungumza na wewe, wapo walimu kutoka Shule ya Nyakunguru wanachimba dhahabu na tunapata fedha nyingi tu.
Lakini cha kushangaza tunapowauliza juu ya kazi yao ya ualimu, wanasema kazi hiyo haina maslahi na serikali imewasahau wanaishi maisha ya tabu, alisema mmoja wa wachimbaji katika mgodi huo.
Aidha, inadaiwa kwamba walimu hao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wanafunzi kwenda kuchimba madini mgodini hapo.
Mmoja wa walimu wa shule jirani ya Nyakunguru A, alithibitisha kuwapo kwa hali hiyo na hata yeye huenda machimboni siku za Jumamosi na Jumapili.
Hata mwenyekiti wa kijiji yupo hapa tunachimba naye dhahabu, na wananchi wenye shida za kiofisi dhidi ya mwenyekiti, wanalazimika kuja huku machimboni kuonana naye, alisema mwalimu huyo. Ofisa Elimu wa Wilaya ya Tarime, Emmanuel Johnson, alipoulizwa kwa njia ya simu juu ya madai hayo, alisema hana taarifa za walimu wake kutimkia machimboni. Mimi sina taarifa juu ya hilo, na anayepaswa kuzungumzia suala hilo ni Mkurugenzi wa Halmashauri kwa sababu ndiye msemaji mkuu wa halmashauri yetu, alisema ofisa elimu huyo.