Walimu wote kukatwa tsh 25,000 ya maabara mwezi october

SODOKA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,656
Reaction score
722
eti jamani huku wilayani kwangu tuemtumiwa sms walimu wote tunakatwa tsh 25 katika mshahara wa mwezi huu kwa ajili ya maabara ktk shule za kata,,,Nahsi ni huku Lindi ktk wilaya moja niliko mie,,,vipi nyie huko mliko na nyie mnakatwa ???
 
walimu wote inabidi mchangie ujenzi wa secondari kwa nch nzima hongera ccm kwa kuwaburudisha walimu wenu
 
kwi kwi kwiiiiiiiiiheheheheee! HONGERA CCM kwa kuwajari wanaotupga kampan ya kuiba kura kwenye vituo vya uchaguzi, nasikia ccm wameanza kuwasumbua mpaka wanakijiji wachangie kla kaya 15000, halafu wanafunzi woooooooote shule za kata wanatakiwa kulipa sh 10000, chezea ccm wewe!. nahapa watendaji wa kata na vijiji wametengenezewa mazingira ya kupiga hela maana ndo wanasimamia hilo zoez, hii ndo ccm bwana halafu kwenye kampen zetu za 2015 tutajinadi kuwa tumejenga maabala na lazima mtuchague :A S wink::A S wink::A S wink:
 
Huu ni uonevu!! kwanini wasichangishwe Raisi, na mawaziri ambao wana mishahara mikubwaa!? kukamua watu wadogo kila siku ni tabia ya shetani hii!!
 
Unaambiwa mwenye nacho ataongezewa na asiye nacho ataporwa hata kile kidogo alichonacho
 
Hela ya kujengea ulitaka itoke kwa nani?,
 
Kwi kwiiiiiiiiiiiii.
Haya maukawa yana tabuu sana. Mbona slaaa na mbowe wanapochangisha M4C kwa walalahoi ili watanulie na mademu zao hamsemi? Ongera serikali kwangu mie chukueni 100000 kwa ujenzi wa maabara wafaidike vizazi vyetu.
 
Ni jambo jema sana serikali kuwakata walimu mishahara. Tena 25,000/- isiwe mwezi mmoja. wakatwe miazi 3 ili seriakli ipate hela za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajli ya maonyesho ya ccm kwenye chaguzi zijazo. Na kwa sababu watanzania wenyewe wakiwamo walimu ni wajinga wajinga tu, watakuwa wakipiga makofi na vigeregere pale wagombea wa ccm Tanzania nzima watakpokuw awakijinadi kwamba ccm imejenga shule na maabara tz nzima na hivyo kuleta maendeleo. Na hili halitakuwa ajabu ikiwa leo hii wanajivunia ujenzi wa barabara kwamba ccm imejenga wakati ni fedha za hao wajinga walalahoi wakiwemo walimu wanazolipa kama kodi, na kwamba hata mishahara ya wafanyakazi wote waliopo na wale wa hewa, wanalipwa na kodi hizi.

Kwa hiyo michango hii isimamiwe na jeshi la polisi ambao wawe na uwezo wa kupita fisi kwa ofisi na kufannya makusanyo ya michango hiyo kama kukata juu kw ajuu itakuwa ngumu.

Wale watakaohoji, wapigwe picha ili waitwe na kamati wahojiwe ili ifahamike adhabu yao sahihi ni ipi kati ya kufutwa kazi, kukolimbwa, kumwangosiwa, kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, ama kung'olewa meno na kucha. Adhabu hizi zitekelezwe mapema kabla hawajaeneza sumu kwa wengine ili wabaki walimu misukule safi isiyo na midomo.

Lingine, ninadhani ni vizuri wakatambua seriakli sasa haina fedha kwa sababu ya matumizi makubwa yasiyotija na sasa inabidi ianze kunyag'anya misharaha ya wafanyakazi ili kuwekeza kwenye mipango ya seriakli ya maendeleo.

Deni la taifa limeongezeka kuliko kiwango na hatukopesheki tena na hivo lazima wachangie ili seriakli iweze kuendeshwa. Bahati mbaya kina Kafulila wameunguza picha na sasa wafadhili wanasita kutupa fedha zingine.

Lakini pia wanatakiwa walimu waonyeshe uzalendo kama washirika wakuu wa serikali ambayo inahitaji kuwa na fedha nyingi kwa ajil ya ccm ili ipate kuhonga vizuri wapiga kura katika chauguzi zijazo.

Kwa weli wlaimu mna mioyo yakuigwa na endeleeni na moyo huo huo!..

Misukule Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!
 
na kura watasaidia kuiba kama kawaida, hadi 2015 watakuta washasahau machungu ya kukatwa hela za maabara.
 
Nini maana ya development plans?

Ni vigezo gani vinatumika katika kupanga kodi kutoka kwa wafanyakazi?

Kiongozi anaporopoka ahadi kwa unafiki na hatimaye anatoa amri ya utelezaji wa maazimio ya kichwa chake ambayo hajui ni namna gani yatafanyika, tafsiri yake ni unyang'anyi wa mapato ya wananchi ambao tayari mzigo wa kodi ni kama gunia la mavi kwao?

Usijiondoe akili hapa kwa kuwa tu wewe siye unayenyang'anywa. Fedha zote hazina seriakli imefasidi, deni la laifa ni kubwa hata seriakli inashindwa kutoa takwimu zozote zinazoonyesha uwiano wa deni hilo na investments na expenditure.
Sasa ccm imekosa pa kuiba ndiyo inaanza uharamia wa kunyag'anya hata kile maskini mwalimu anakipata? Huu si wenda wazimu?

Ujinga wa kutozingatia priorities kwenye budgets, kutumia fedha kifisadi bila kufuata mipango iliyowekwa, kuuropoka aahdi kwa ajili ya aibu, haitakiwi athari zake arundikiwe mwalimu ama mfanyakazi.

Kwa kuwa hayo ni mahitaji ya dharura ya ccm, ccm i finance angalau ujenzi huo wenye lengo zuri lakini dhamira ni ya kinafiki.

Huu ni uharamia, ujangili na upumbavu!.

Hela ya kujengea ulitaka itoke kwa nani?,
 
eti jamani huku wilayani kwangu tuemtumiwa sms walimu wote tunakatwa tsh 25 katika mshahara wa mwezi huu kwa ajili ya maabara ktk shule za kata,,,Nahsi ni huku Lindi ktk wilaya moja niliko mie,,,vipi nyie huko mliko na nyie mnakatwa ???

Hizi ni shidaaa kwanini wasingewakata wajumbe wa bunge maalumu la katiba (BMK) hizo hela
 
Halafu ukisikia kiongozi katoa ahad anaenda kuchukua hela ofisi ya serikali ndiyo anachangia ww unatoa kwenye mshahara wako na unakata
Loan board
NMB
Baiport
Saccos
 
Halafu ukisikia kiongozi katoa ahad anaenda kuchukua hela ofisi ya serikali ndiyo anachangia ww unatoa kwenye mshahara wako na unakata
Loan board
NMB
Baiport
Saccos

umesahau oppotunity .faidika.cjui finka. dawa yao ni moja 1.piga panga msosi wa wanafunzi 2 kuuza chemical maabara ikijengwa nakuandikia watoto walifanya practical.3 .kila mwanafunzi alete mayai 4 yakufanyia food taste 4 na mengine kama hayo hadi kila mtu ajilipe 25000 yake na 20000 ya usumbufu
 
WAALIMU mmekua makondoo sana!mmeshindwa hata kupigania TANZANIA TEACHERS COMMISSION ikaanzishwa ktk katiba mjiandae ccm kuwapuuza haswa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…