Walimu wote kukatwa tsh 25,000 ya maabara mwezi october

Walimu wote kukatwa tsh 25,000 ya maabara mwezi october

Mtumishi hawezi katwa mshahara wake bila ridhaa yake ama maridhiano na mwajiri. Ni kosa kisheria.
 
Huu ni uongo. DED - Sekondari wa Sumbawanga amekuja shuleni kutuomba tuchangie kwa hiari, na kusema mwajiri hawezi kukata mshahara wa mtu. Alisema haiwezekani mtu kukatwa 25,000 nchi nzima ili hali kiwango cha kuchangia kinatofautiana. Pia, kuna baadhi ya watumishi wamekwisha lipa kwenye maeneo yao.
Alionya ya kwamba sheria na kanuni za maeneo husika zinaweza kutumika kumwadhibu mtumishi, ila si ,wajiri.
Kinyume na kawaida yake, aliongea kwa upole kabisa, akitusihi tuchangie hata shilingi 2,000/-, huku wananchi wakichangishwa 15,000/-.
Tusubiri
 
Ni jambo jema sana serikali kuwakata walimu mishahara. Tena 25,000/- isiwe mwezi mmoja. wakatwe miazi 3 ili seriakli ipate hela za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajli ya maonyesho ya ccm kwenye chaguzi zijazo. Na kwa sababu watanzania wenyewe wakiwamo walimu ni wajinga wajinga tu, watakuwa wakipiga makofi na vigeregere pale wagombea wa ccm Tanzania nzima watakpokuw awakijinadi kwamba ccm imejenga shule na maabara tz nzima na hivyo kuleta maendeleo. Na hili halitakuwa ajabu ikiwa leo hii wanajivunia ujenzi wa barabara kwamba ccm imejenga wakati ni fedha za hao wajinga walalahoi wakiwemo walimu wanazolipa kama kodi, na kwamba hata mishahara ya wafanyakazi wote waliopo na wale wa hewa, wanalipwa na kodi hizi.

Kwa hiyo michango hii isimamiwe na jeshi la polisi ambao wawe na uwezo wa kupita fisi kwa ofisi na kufannya makusanyo ya michango hiyo kama kukata juu kw ajuu itakuwa ngumu.

Wale watakaohoji, wapigwe picha ili waitwe na kamati wahojiwe ili ifahamike adhabu yao sahihi ni ipi kati ya kufutwa kazi, kukolimbwa, kumwangosiwa, kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, ama kung'olewa meno na kucha. Adhabu hizi zitekelezwe mapema kabla hawajaeneza sumu kwa wengine ili wabaki walimu misukule safi isiyo na midomo.

Lingine, ninadhani ni vizuri wakatambua seriakli sasa haina fedha kwa sababu ya matumizi makubwa yasiyotija na sasa inabidi ianze kunyag'anya misharaha ya wafanyakazi ili kuwekeza kwenye mipango ya seriakli ya maendeleo.

Deni la taifa limeongezeka kuliko kiwango na hatukopesheki tena na hivo lazima wachangie ili seriakli iweze kuendeshwa. Bahati mbaya kina Kafulila wameunguza picha na sasa wafadhili wanasita kutupa fedha zingine.

Lakini pia wanatakiwa walimu waonyeshe uzalendo kama washirika wakuu wa serikali ambayo inahitaji kuwa na fedha nyingi kwa ajil ya ccm ili ipate kuhonga vizuri wapiga kura katika chauguzi zijazo.

Kwa weli wlaimu mna mioyo yakuigwa na endeleeni na moyo huo huo!..

Misukule Hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!

Naomba kuuliza!Walimu na watanzania ni mijingamijinga tu umesema.Katika hiyo mijingamijinga ujue na baba,mama,shangazi na wajomba zako wamo wakiwa kama watanzania.Nakushauri kama una busara waombe radhi hao wazazi wako uliowatusi na siku nyingine usirudie kutukana wazazi wako.Sisi wengine huku tushakushusha thamani kwa kutokuweza kufikiri sawasawa ktk haya matusi.Kweli utubusara-ujingahasara.
 
CCM booombaaaaaa...hiko kiwango mbona ni kidogo sana? tufanyieni 50,000 kwa miezi mitatu mfululizo ili mshibe vizuri.
 
Thamani yangu haitegemei maamuzi ya akili yako. Nafasi hiyo huna na hata uwezo wa kuni rank in anyway naona huna.

Msamaha siombi kwa sababu mimi si mnafiki. Na halafu niliyoandika ndio ukweli na ukweli mtupu. Watanzania hasa walimu ni wajinga wajinga tu. Na ujinga siyo tusi bali ni sifa ya mtu asiyefahamu mambo anayopaswa kuwa ameyafahamu. Kosa langu ni kuwa mkweli?

Zaidi sana huwezi kuni blackmail kwa kuwafanya wazazi wangu human shield for your pride.

Naona unajua kusoma, sijui kama unajua na kuandka lakini ni dhahiri hujui kuelewa.



Naomba kuuliza!Walimu na watanzania ni mijingamijinga tu umesema.Katika hiyo mijingamijinga ujue na baba,mama,shangazi na wajomba zako wamo wakiwa kama watanzania.Nakushauri kama una busara waombe radhi hao wazazi wako uliowatusi na siku nyingine usirudie kutukana wazazi wako.Sisi wengine huku tushakushusha thamani kwa kutokuweza kufikiri sawasawa ktk haya matusi.Kweli utubusara-ujingahasara.
 
Huu kweli uonevu. Mwalimu analipa kodi Mara mbili kila mwezi, analipa modi anaponunua bidhaa sokoni na anakatwa kodi na serikali. Inamaana kodi yote hii haitoshi kujengea maabara? Au serikali inataka kuwafanya walimu wajute kusomea fani hii?
 
Back
Top Bottom