KERO Walinzi tuliosimamia Mitihani ya Taifa Form 4 - Kakonko tumelipwa posho pungufu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Walinzi tuliosimamia Mitihani ya Taifa Kidato cha Nne, Wilaya ya Kakonko tumepewa malipo yasiyoendana na siku za kazi yenyewe, tunakaa na mitihani siku 7 ila malipo tuliyopewa yalikuwa ya siku tano.

Malipo hayo ni Sh 75k kwa siku, wengine vituo tulivyoenda kusimamia vilikuwa vya mbali na kutoka kwenye makazi yetu, lakini Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya anatupa malipo pungufu.

Kungetokea shida wa kwanza kuwajibishwa ingekuwa ni sisi walinzi lakini tumesimama kwa nguvu zote kutimiza majukumu yetu kisha tunalipwa pungufu.
 
Sio Tuliosimamia, Sema Tunaosimamiaa, Kwasababu Mitihani Bado inaendeleaa....
 
Hamna mawasiliano na mkurugenzi?
 
Ndiyo maana nilimuita yule jamaa mwehu,DED mapesa mengi sana yanapita kwake kuliko boss wake DC!!

BTW: Subiri na wasimamizi wanakuja kuungana nawe kulialia muda si mrefu.
 
Subiri mshahara bana wacha kutuchosha na malalamiko yako yasiyo na kichwa wala miguu

Posho huwa haipangwi posho unapewa chochote kilichopo ata mngepewa sahani za wali marage zilikua zinatosha

Kwanza mnalinda nn
 
Semeni mama anaupiga mwingi hela zitaingia kwenye akaunti zenu muda huohuo.
 
Ni tatizo la nchi za Africa, bila upigaji mtu haridhiki. Zimeingia tumboni mwa mtu!!
 
Tumelichukua Tutalifanyizia Kazi Ili Mhasibu Ajue Kuwa Pesa Za Watu Zitatokea Ndugu Lolote Lililowazi La Mwili Wake ⏰️ Watu Wamevuja Jasho
 
Walinzi tuliosimamia Mitihani ya Taifa Kidato cha Nne, Wilaya ya Kakonko tumepewa malipo yasiyoendana na siku za kazi yenyewe, tunakaa na mitihani siku 7 ila malipo tuliyopewa yalikuwa ya siku tano.
Zile bunduki walizowapa 29 October si mnazo? Wageuzieni wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…