Walinzi tuliosimamia Mitihani ya Taifa Kidato cha Nne, Wilaya ya Kakonko tumepewa malipo yasiyoendana na siku za kazi yenyewe, tunakaa na mitihani siku 7 ila malipo tuliyopewa yalikuwa ya siku tano.
Malipo hayo ni Sh 75k kwa siku, wengine vituo tulivyoenda kusimamia vilikuwa vya mbali na kutoka kwenye makazi yetu, lakini Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya anatupa malipo pungufu.
Kungetokea shida wa kwanza kuwajibishwa ingekuwa ni sisi walinzi lakini tumesimama kwa nguvu zote kutimiza majukumu yetu kisha tunalipwa pungufu.