Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Wakuu salamu
Mimi Mfanyakazi kutoka Kampuni ya China Tanzania Security (CT) ambayo inahusika na usimamizi wa miundombinu katika Vituo vya Mabasi ya Usafiri wa Haraka (Mwendokasi) (DART) pamoja na usalama wa abiria wanaopata huduma kupitia vituo tunavyohusika navyo ikiwemo Mbezi Luis, Kimara na Gerezani.
Nikiwa nawakilisha wenzangu wengi naleta hoja yangu kwa masikitiko makubwa, ni kwamba sasa ni miezi mitatu imepita bila Wafanyakazi kulipwa stahiki zetu yaani mshahara, tunaishi kwa tabu sana takribani Wafanyakazi 200 wote kilio chetu ni kimoja.
Tumejaribu kufuatilia hata kwa viongozi ikiwemo kwa HR lakini hatupati majibu yanayoeleweka huku siku zikiendelea kusonga, tunaofuatilia zaidi tunaambiwa kama hatuwezi kufanya kazi na kampuni hiyo basi tukabidhi mavazi ili tuache kazi.
Lakini changamoto kubwa nyingine tunayokutana nayo kwenye kampuni hii, wamekuwa wagumu kutoa mikataba ya maandishi badala yake wanatoa mikataba kwa midomo huku wakiahidi kutoa ya mikataba kwenye maandishi lakini hawafanyi hivyo ni danadana tu, mfano mimi binafsi nimefanya kazi takribani miaka miwili na kampuni hiyo lakini sijawai kupewa huo Mkataba wa maandishi.
Tunaomba tusaidiwe katika hayo, wengi tunafahamu kwa maisha ya Dar es Salaam bila kulipwa fedha kwa miezi mitatu maisha na Mtu ana familia hali inavyokuwa ngumu.
Hali hii inaweza kupelekea wengine kuanza tabia za udokozi au wizi kwenye maeneo yao ya kazi licha ya kuwa sisi ndio tunategemewe kuhakikisha usalama wa miundombinu na mali za abiria vinakuwa salama, tunaweza kujiuliza usalama unapatikanaje kama watu hawalipwi stahiki zao.
Wito wetu kwa wahusika tunaomba watulipe pesa zetu zote lakini kama inawezekana mamlaka husika ziwafuatilie kwa ukaribu zaidi ili vitendo hivi visiendelee kwa kuwa vinakiuka haki za wengi na kuongeza mazingira ya hofu kwa wafanyakazi walio wengi.
UPANDE WA KAMPUNI
JamiiForums imewasiliana na Afisa wa Kampuni hiyo, Berry Makoyola, alipoelezwa kuhusu madai hayo amesema:
“Nimesikia na nimeelewa ila siwezi kujibu hoja hizo, nitaziwasilisha kwa mhusika ambaye ana mamlaka ya kutoa majibu ya Kampuni kuhusu madai hayo.
Majibu ya Kampuni soma hapa ~ Kampuni ya China Tanzania Security yafafanua madai ya Walinzi wa Vituo vya Mwendokasi kutolipwa mishahara ya miezi mitatu
Pia soma ~ Upigaji, utapeli, uliojifichika kwenye kofia ya Kampuni Binafsi za Ulinzi