Walinzi tunaosimamia Vituo vya Mwendokasi hatujalipwa mshahara kwa miezi mitatu, tukifuatilia tunapigwa danadana

Walinzi tunaosimamia Vituo vya Mwendokasi hatujalipwa mshahara kwa miezi mitatu, tukifuatilia tunapigwa danadana

sasa mnashindwa nini kugawana mbao? kama nyie ndio mnasimamia kila kitu kwanini msichukue makusanyo ya nauli kwa siku mkajilipa then msepe? nyie wawapi askari mnalalamika kama raia hii mbona haijakaa sawa.
Wao ni walinzi tu ni sawa na Walinzi wa Bank au Stand au Sokoni.
 
Poleni sana vijana nilikuwa na swahiba alikuwa anafanya kazi kampuni iyo mshahra 150k ukitega ni inalambwa 10k,mwanzo nafikiri walikuwa wanalipa vizuri sijajuwa ni financial crisis imewakumba au vip, watu wanafanya lazi kwasababu watafanyaje kuliko kukaa bure.
 
Hela yenyewe ndogo ,maisha magumu,bado kuna mtu anasumbua kulipa watu kwa wakati mpaka waanze kudai haki yao alafu muwaite wakorofi.
Laana nyingine zinaanzia huku.😥😢😢
 
Hali hii inaweza kupelekea wengine kuanza tabia za udokozi au wizi kwenye maeneo yao ya kazi licha ya kuwa sisi ndio tunategemewe kuhakikisha usalama wa miundombinu na mali za abiria vinakuwa salama, tunaweza kujiuliza usalama unapatikanaje kama watu hawalipwi stahiki zao.
Kwa hiyo mkuu tunavyowaona pale kituoni na matumbo yenu makubwa hamjalipwa miezi mitatu? Ndiyo maana mmeanza kula rushwa ya kuingiza watu kwenye wale wa mahitaji maalum?
 
Hawa CT hawana hata day off ni mwendo wa naandika bandua mshahara wao ni 150000 wana makato mia kidogo yaani akichelewa kidogo kuingia kazini anakatwa akikutwa kasinzia kidogo kakatwa na hawana overtime likizo yenyewe kwa mbinde sana kwa hiyo net salary unaweza kuta anaondoka na 80 au 90 ukweli wanahitaji watu wa kuwasemea
 
Back
Top Bottom