Walinzi wa mwili wa Putin ‘hukusanya kinyesi chake anaposafiri nje ya nchi na kukirudisha Urusi pamoja naye’

Walinzi wa mwili wa Putin ‘hukusanya kinyesi chake anaposafiri nje ya nchi na kukirudisha Urusi pamoja naye’

Kwenye misafara ya Samia kuna wabeba mavi kumbe? Si kwa ukubwa wa misafara yake ile.

Rais wa Africa hawezi kurudi nyumbani na choo

Wakiugua kidogo wanaenda Ulaya, cha kwanza "Mheshimiwa tunaomba choo"!

Jamani ni upele usoni, mbona sijawahi kuulizwa choo, "Mama, Madaktari wako ni fambo ndo maana umekuja kwetu, tunaomba choo please" !

Jamii tegemezi, hau train watu wako, hununui vifaa tiba, utaificha nini dunia.

Hakuna kitu cha ajabu duniani kama kiongozi wa Afrika anapoenda Ulaya kutibiwa
huku kwa kutumia pesa ya wale anaotakiwa kuwajengea hospitali.
 
Kawaida huwa wanatembea na vyoo marais wote duniani
Upekee wa putin, kim na trump wao hata wanapoenda nje ya mabara wanavyo na ajabu zaid wao vinyesi vyao havitupwi huko huko wanarudi navyo



Wakati wengine vinatuowa hukohuko mfano rais wa taifa lenu huko africa nk
 
realratedred Vladimir Putin anakutana na Donald Trump huko Alaska leo kwa mazungumzo ya amani yenye umuhimu mkubwa kuhusu vita vya Ukraine, na inaripotiwa kwamba ameambatana na moja ya hatua zake za kiusalama za ajabu kabisa.

Kulingana na waandishi wa habari wa uchunguzi kutoka Ufaransa, Regis Gente na Mikhail Rubin, wanachama wa Huduma ya Ulinzi ya Shirikisho la Putin wamepewa jukumu la kukusanya taka zake zote za mwili, ikiwemo kinyesi, kila anaposafiri nje ya nchi. Taka hizo hufungwa kwenye mifuko maalum na kusafirishwa kurudi Urusi kwenye begi maalum. Sababu inayodaiwa? Kuzuia mashirika ya kijasusi ya kigeni kupata sampuli ambazo zinaweza kufichua maelezo kuhusu afya ya Putin.

Inasemekana utaratibu huu umekuwepo kwa miongo kadhaa, huku tahadhari kama hizi zikichukuliwa pia wakati wa ziara nchini Ufaransa, Austria, na nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na vyoo maalum vya kubebeka vinavyoletwa kwa ajili ya matumizi yake pekee.

Uvumi kuhusu afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 72 umechochewa na muonekano wake wa hadharani unaoonyesha kutetemeka, kuruka kwa mguu, na taarifa ambazo hazijathibitishwa kuhusu kuanguka, matatizo ya moyo, na hofu za kiafya za neva.
Hiyo kawaida tu mbona
 
Back
Top Bottom