acheni ujuaji kwenye ulinzi wa mkuu wa nchi,
mleta mada elewa kuwa ulinzi wowote hasa wa mtu mhimu kama rais uko katika ringi 'ring' kuu tatu mhimu hasa kulingana na mazingira aliyopo mlindwa(esp.rais)
1.Ringi ya tatu.
hii ni ringi ya nje ambayo ndio nguzo mhimu kabisa kwenye ringi zote zilizobaki, ringi hii inajumuisha nguvu kazi ya wanausalama hasa wa intelijensia ambao kazi yao kuu ni kunasa au kupeleleza usalama wa mazingira yaliyo karibu na rais na kutuma taarifa kwenye ringi ya kwanza na ya pili kupitia redio maalum za kiusalama ( huonekana wazi kwenye sikio mojawapo kwa walinzi kama earphone hivi) katika hali tulivu ringi hii haijumuishi silaha nzito bali ni nyepesi kama bastola n.k ila ktk hali isiyo salama huhusisha silaha nzito za kujihami aghalabu submachines kama UZI, AKs (fupi sana) n.k
2.Ringi ya pili
hii ni co-ordination ring kati ya ringi ya tatu na ya kwanza, ringi hii huundwa na kikosi cha kujihami na kushambulia chenye nguvu kazi ya maafisa wachache wenye uwezo wa juu kimapambano ( ELITE PERSONNELS), kazi kubwa ya ringi hii ni kupokea taarifa kutoka C yaani ringi ya 3 na kuzifanyia kazi iwapo inahitajika, mfano mhalifu anaweza kuhisiwa na ringi ya 3 na hivyo ringi ya 2 hujulishwa ili kuchunguza au kureact directly kwa adui, mfano adui anapohisiwa mkutanoni ambapo rais anahutubia nguvu kazi kutoka ringi ya pili humsogelea adui na kukaa naye karibu( kwenye kundi la watu) ili kuweka urahisi wa ku intercept mashambulizi kutoka kwa huyu adui, hii huundwa na nguvu kazi yenye uwezo mkubwa katika medani za kivita na intelijensia mf commandos.
1.Ringi ya kwanza,
Ringi hii ndio iliyozoeleka kuonekana machoni pa wengi, ni ringi inayojumuisha wanaoitwa 'VIP BODYGUARDS' ringi hii humjumuisha mpambe wa rais yaani ADC na nguvu kazi ya wabobezi wa close combat ambao ni commandos, kazi yao kubwa kudhibiti any physical contact kwa rais, wako alerted sana na hupokea miongozo toka kwa wanausalama toka ringi ya 2, na 3, kupitia redio,
Pia iwapo kutatokea fujo au jaribio kumdhuru kiongozi ringi hii hufanya kazi ya uokoaji ( rescue unit) na kumuondosha rais eneo hilo huku wakijbu mapigo na kuondoka nae huku wakiiacha ringi ya pili ikiendelea kudhibiti tishio kwa mapigano ya silaha, endapo mapigano hayo yatakuwa magumu ringi ya pili huhitaji msaada kutoka vyombo vingine vya usalama kama polisi na jeshi.
ikumbukwe kuwa ringi hii ya kwanza pia hubeba silaha ndogo(portable) zenye ufanisi zaidi.
ULINZI WA RAIS SI SUALA JEPESI WALA NADHARIA ZA KISIASA, NI UTENDAJI HALISI
Nb; RINGI HIZI NI KULINGANA NA HALI, SIFA, YA ENEO HUSIKA INAWEZA IKAZIDI HAPO
THAKS, HAVE IT THOUGH SOME OF IT!