Walinzi wa Suma JKT hawajui wajibu wao

Walinzi wa Suma JKT hawajui wajibu wao

Acha kuwapa kichwa hao wajinga.

BODABODA zinaua watu kila siku na bado wanazipanda. Hao JKT Kama wanaua watu sio sababu ya kuwaogopa. Ndio maana mnarogwa sio kila mtu ni wa kupelekeshwa.

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
Siwapi kichwa ila natetea uhai wa jamaa, wale watu wana stress ukiingia 18 zao wanakuua
 
Ha ha ha

Nashukuru MunGu mimi huwa nawaita ASKARI

Tena niwafundishe jambo kuanzia leo popote utapomkuta Suma jkt muite kwa jina la ASKARI utanishukuru

Kuna muda inabidi tuwafurahishe watu wenGi bila kujali wewe ni nani

Maarifa
 
Jipime ubavu ukiona una mmudu unauwasha moto tu unamchakaza ila ukiona hautoki labda wapo nyomi unakula gundi tu unatemana nao
Maana ni ujinga kupambana vita unayojua utashindwa

Alaf busara ni kuepusha mzozo na mjinga na ukiuanzisha mzozo na wajinga na wewe unakua ni mjinga pia, kwahiyo siku nyingine we waite tu askari utaepusha mengi
 
Stress za kutaka kuwa Wanajeshi zinawaumiza, kiukweli hawa SUMAJKT wanalalamikiwa kwenye taasisi nyingi sana kwa vitendo vyao
 
Hapo kweli walinzi wamezingua,halafu hao walinzi wa Suma JKT Wana Tatizo Gani maana watu Wana malalamiko mengi sana kuwahusu Hiyo kampuni ijiangilie maana raia washaanza kuwasagia kunguni mitandaoni
Wasipochukua hatua watajua hawajui Kwa biashara Yao!
Walijiunga JKT ili waje kuwa wanajeshi sasa wamekuja kuangukia kwenye Ulinzi ndio kinachowafanya wawe hivyo
 
Mlinzi ni babu masai tu , hao waliopitia mafunzo ukiwajumlisha na Garda na hizo security companies nyingine + hao suma JKT wote ni askari ‘kitaalamu hiko hivyo.

Sisi tu watanzania na tabia zetu mbaya ndio tunawaita walinzi.
Unaweza kuelezea japo kwa sentesi mbili tofauti ya mlinzi na askari. pia itapendeza ukiongezea majukumu ya kila mmoja asante
 
Aisee jana nimeponea chupuchupu kuzirusha na Walinzi wa SUMA JKT, ipo hivi mimi ni dereva Bajaj sasa kuna abiria wangu huwa nampeleka ofisini na kumfata, jana akaniambia kapata dharura haendi kazini ila akanipa laptop nipeleke ofisini kwao na namba ya muhusika ambaye anatakiwa kupelekewa hiyo laptop akanipa, nilipofika pale nikampigia simu akaniambia ametoka kidogo hiyo laptop niwaachie Walinzi hapo getini nilivyo maliza kuongea na simu kuna mlinzi wa kike akaniuliza kasemaje?

Nikamjibu kasema niwaachie nyie Walinzi anakuja kuichukulia hapa aisee yule mdada akaanza wewe usirudie tena kutuita Walinzi, nikauliza nyie ni wakina nani?

Akawa ananiambia uwe na heshima usitake kubishana na mimi tukazozana pale wale wengine nao wakaingilia nikawaambia nyie ni Walinzi kama hamfanyi kazi ya ulinzi ondokeni hapa mmoja akamwambia wenzake eti huyu ni wakumpa materials za kijeshi Ili atuelewe nikawaambia hilo haliwezekani mkitaka kuhatarisha ajira yenu mniguse kisa nimewaita Walinzi nikawasha zangu Bajaj nikaondoka.

Nilishangaa sana hawa jamaa sijui ndivyo wanavyoambiwa huko na wakubwa zao au ni uelewa mdogo.
Nadhani viongozi Suma JKT inabidi wajitafakari endapo ile mbeleko ya kubebwa na serikali kulinda taasisi zake itatupwa hawatoweza kupewa tenda ya kulinda mahali popote.
 
Sasa kama wao sio walinzi ni akinani.?

Hio kampuni imeshafeli
 
Ndugu yangu nakusihi usibishane nao siku nyingine watakupiga wakuue, sio kwamba nawaogopa hapana ila hata mimi nilikuwa mlinzi wa Suma Jkt. Kilichopo ni kuwa wengi wa wale walinzi ni vijana kutoka jkt ambao wengi tulikuwa na matumaini ya kuajiriwa na jwtz kwa hiyo unapomuona pale getini sio kwamba kapenda kufanya kazi ile hapana ni kukosa tu kazi kwa hiyo anaishi katika msongo wa mawazo.
Sasa wewe jichanganye hasira zao wakumalizie wewe, kila siku unasikia watu wanauawa na hao sumajkt halafu wewe unajipeleka tu. They have nothing to loose.
Hawana maajqnu yeyote nilipita JKT usiwatishe watu.

Wengi wao wapuuzi tu hawana reasoning
 
Mlinzi ni babu masai tu , hao waliopitia mafunzo ukiwajumlisha na Garda na hizo security companies nyingine + hao suma JKT wote ni askari ‘kitaalamu hiko hivyo.

Sisi tu watanzania na tabia zetu mbaya ndio tunawaita walinzi.
Kwani askari kazi yake ni nini mkuu? Sio kulinda!
Na mtu anayelinda ni mlinzi.
Hata wanajeshi, polisi,n.k ni walinzi.
 
Kwani askari kazi yake ni nini mkuu? Sio kulinda!
Na mtu anayelinda ni mlinzi.
Hata wanajeshi, polisi,n.k ni walinzi.
Ni kweli Copy, ila shida ni ile kumuita mlinzi.
Binafsi naitaga tu afande nimejizoelea hivyo tokea nasoma… yan nimkute MP getini nimwambie eti shikamoo mlinzi? Kisa yupo getini anakagua wanafunzi tunaopita? Si nitakula doso mpaka niishiwe pumzi 🤣🤣
 
Aisee jana nimeponea chupuchupu kuzirusha na Walinzi wa SUMA JKT, ipo hivi mimi ni dereva Bajaj sasa kuna abiria wangu huwa nampeleka ofisini na kumfata, jana akaniambia kapata dharura haendi kazini ila akanipa laptop nipeleke ofisini kwao na namba ya muhusika ambaye anatakiwa kupelekewa hiyo laptop akanipa, nilipofika pale nikampigia simu akaniambia ametoka kidogo hiyo laptop niwaachie Walinzi hapo getini nilivyo maliza kuongea na simu kuna mlinzi wa kike akaniuliza kasemaje?

Nikamjibu kasema niwaachie nyie Walinzi anakuja kuichukulia hapa aisee yule mdada akaanza wewe usirudie tena kutuita Walinzi, nikauliza nyie ni wakina nani?

Akawa ananiambia uwe na heshima usitake kubishana na mimi tukazozana pale wale wengine nao wakaingilia nikawaambia nyie ni Walinzi kama hamfanyi kazi ya ulinzi ondokeni hapa mmoja akamwambia wenzake eti huyu ni wakumpa materials za kijeshi Ili atuelewe nikawaambia hilo haliwezekani mkitaka kuhatarisha ajira yenu mniguse kisa nimewaita Walinzi nikawasha zangu Bajaj nikaondoka.

Nilishangaa sana hawa jamaa sijui ndivyo wanavyoambiwa huko na wakubwa zao au ni uelewa mdogo.
Mngepigana tu ila tuone Nani Ni kamanda.

Wabongo tuko vizuri kwenye kushabikia
 
Back
Top Bottom