Walinzi wa SUMA JKT mmekuwa Kero sana au ni stress za kukatishwa ndoto za kuwa JWTZ

Walinzi wa SUMA JKT mmekuwa Kero sana au ni stress za kukatishwa ndoto za kuwa JWTZ

Mshahara wa laki 2 utafaa nini mkuu?
Hapo take home 180K, kama unakuwa uko vizuri saidia tu wana maisha magumu.
SUMA ni shirika la Serikali (JKT) lakini kinachofanyika ni zaidi ya unyonyaji.

Jamaa yangu mmoja aliwahi kuniambia Shirika linatoza si chini ya 500K kwa mlinzi mmoja lakini mlinzi huyo anaambulia 180K kama take home ikiwa ni baada ya makato ya NHIF

Shame on you SUMA management

Dah
 
Mimi niliingia library wakati natoka Suma jkt mmoja apo reception akaniuliza unatafuna nn ?nikamwambia natafuna meno,akasema tema unachotafuna nikatema big gee,nikaondoka zangu,
 
Huwa wanajihisi JW wakiwa magetini [emoji23][emoji23][emoji23]. Wanakera sana hawa "walinzi" wamagetini. Wanatumia nguvu kubwa kwa ishu ndogooo
 
Pale Bugando kuna mmoja alinizuia eti matunda siyo chakula anataka waingie walio na chakula tu. Nilijiuliza sana mgonjwa wangu anahitaji matunda jamaa kakaza hakuna kuingia.

Ujingaujinga tu na stress zao hawa vijana wa SUMA
[emoji23][emoji23][emoji23] Mkuu pole sana, kumbe nilikukera. Ntajirekebisha.
Joke sio mimi bana
 
Kumbe ni sehemu nyingi wanasumbua.

Pale Mtera Hydro Power Station barabara ya Dodoma-Iringa kwenye mageti wanaombaomba sana kama hawalipwi mishahara vile ukipita na private car utasikia kaka au dada hatupati hata hela ya maji? wanakera sana.
Hapo mtera ni mabingwa wa kuomba omba

Kuna siku nikajipanga nikasema leo hata iweje sitoi chochote kwao, maana wanaudhi ,na kweli kila alichoomba kuanzia maji ya kunywa hadi pesa ya kahawa nikamwambia sina , ebana ee kuna pakti ya karanga nilikuwa natafuna akaiona , ! Nasikia broo kama vip nipe nimalizie hizo karanga !!!

Mtera kwa kuomba ni next level

Sent from my RMX3085 using JamiiForums mobile app
 
wale wa kike wamekuwa wadangaji tu. full kuomba hela. basi na mimi natafuta mmoja aliyenona nampa anachotaka
 
Kwani Suma jkt ,wamekufanya nini broh? mbona umekomaa nao sana... negatively.. Hivi suma jkt na CCM bora nini?
Hao CCM wenyewe tu wamewakimbiza sumajkt kwenye mwendokasi bimkubwa kasema hawa wapuuzi wanaweza nigombanisha na wananchi bure Sasa hivi hawapo busara hawana wale
 
Baadhi wana mambo ya kiwaki mfano mmoja nlimkuta FIRE Dart ila haifai kuwadharau wale ni wadada wamama wababa na wakaka wa familia za watanzania wenzetu
RIDHIKI ISITUJAZE KIBRI
 
Back
Top Bottom