Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kama dr. Slaa anaitumia barua hii kama msingi wake wa malalamiko, hapo ameshashindwa na ikienda mahakamani hii barua itamwumbua sana.
Huhitaji hata kuwa na akili kubwa kujua hiyo barua ni fake. Na ikienda mahakamani itachambuliwa kama njugu.
Ubaya wa mahakama, wakigundua umetoa barua fake, madai yako mengine yote hata yale ya maana yanatupwa.
Hili la barua hii pamoja na lile la kontaina lenye kura fake huenda slaa alitegeshewa makusudi na wajanja ili waanze kuthibitisha ni muongo na mropokaji.
Kibaya mwandishi ametaja na sehemu walipokutana. Mtu mmoja au wawili wakiwa na alibi kuonyesha isingeliwezekana wawe mwanza wakati huo, madai yote yanaporomoka hapo hapo.
Moderators naomba mtuwekee ile barua tena coz wengine hatukuiona!!
Kinachonitia wasiwasi ktk barua hii ni vipi Rithwaan anaweza kukaa na vigogo namana hiyo, yeye anaposition gani ya kumfanya akae nao meza moja ktk mambo ya chama ( japo bosi wake ktk immar advocates ndiye mwenye jiimbo), japo alikusanya signature za baba yake ktk uteuzi wa CCm kwa babayake. Halafu kwanini iwe ni mwanza tu, wakati chadema ilikuwa na nguvu karibia miji youte mijini (Arusha mjini, Moshi Mjini, ubungo,kawe, Mbeya na Iringa mjini nk) tatu uenyeji wa uandishi wa barua yenyewe ,watu wametajwa ni wale wale ambao kila mtu hataki kuwasikia, asa rostam na mwanza ilemela yeye inamuhusu nini? jamani naomba tuichambue barua hii ili tuweze kupata mwafaka, naomba maoni yenu