Asasi za kiraia, juna jambo kumbwa nyuma ya pazia UDOM!
Jifanye ingalikuwa ni mwanao wa kuzaa na umempeleka akasome chuo kikuu hahafu akaingiliwe kimwili na polisi dhalimu, enzi hizi za UKIMWI, nako pia mtu utaendelea kuonyesha 'UZALENDO' kuifichia serikali kufuru la aina hii au ni kwa sababu tu ni watoto wa wenzenu?
Haki za binadamu mko wapi jambo zito chuo kikuu cha Dodoma mpaka kije kiibuliwe na masharika ya nje tu au mpaka huyo O'Campo tunayemsikia.
Kweli ndio aina ya taifa tunalolijenga kwa kuficha madhambi yanayotisha hivi uvunguni? Wanafunzi wabakwe, wambukizwe magonjwa na watishwe kutokusema halafu nyinyi mpote ai mbaka kuletewa mezani?