Waliobarikiwa hukopesha, kamwe hawanuki madeni, tubadili mtizamo

Waliobarikiwa hukopesha, kamwe hawanuki madeni, tubadili mtizamo

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom.

Kuna Msanii mmoja Jina silijui, ameimba wimbo usemao,
" Sisi ndio wale waliobarikiwaaa na na Mungu." Nakubaliana naye 100%.

( Kumbukumbu 15:6)
"Kwani BWANA, Mungu wako atakubarikia, kama alivyokuahidi,nawe UTAKOPESHA, mataifa mengi, lakini hutakopa, tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao."

Naongea nawe Mtanzania mwenzangu, unayemcha Mungu, Badili mtizamo, Anza kukopesha usidaiwe.

Katika level ya nchi pia, twende hivyo hivyo, Si vyema kujivunia madeni ndugu zangu, watatunanga!!

Tukibadili msimamo huu, tutakwenda vizuri, tukiwa na mtizamo wa kitajiri, huu wizi na ubadhirifu wa Mali ya umma utakoma, ni Umaskini wa mawazo tu ndio unawasumbua Hawa wezi wa Mali za umma!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA. 🇹🇿
Amen

Karibuni!!
 
Umebarikiwa sana Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Kamwe hustahili kunuka madeni!!
 
Yesu alikuwa anakopesha kina nani ? Na ukikopesha unadai au unatoa Hisani ?
 
Ni oweli. KUKOPA ni fedheha.
Niliwahi kwenda ziara kijiji kimoja,

Familia wamepanga matofali yanayofanana usawa wa kitanda chumba Cha kulala watoto.

Ulipofika usiku watoto walichelewa kulala sababu shuka ya kujifunika juu ya kitanda Cha matofali ni koti la baba Yao.

Nilipogundua Hilo, nilifadhaika sana.

Katika Hali hiyo, unasikia inaripotiwa katika vyombo vya habari Eti mkurugenzi Kaiba pesa ya 1.2 bilion iliyotokana na MIKOPO!!

Huu ni Umaskini wa Akili.
 
  • Mshangao
Reactions: G4N
Yesu alikuwa anakopesha kina nani ? Na ukikopesha unadai au unatoa Hisani ?
Yesu hakuwahi kuwa na madeni.

Yeye hakuwa akikopesha tu, aligawa Bure kabisa, uponyaji, Uzima nk nk!!

Kudaiwa, haijawahi kuwa Moja kati ya siha njema hata kidogo.
 
Yesu hakuwahi kuwa na madeni.

Yeye hakuwa akikopesha tu, aligawa Bure kabisa, uponyaji, Uzima nk nk!!

Kudaiwa, haijawahi kuwa Moja kati ya siha njema hata kidogo.
Madeni sio Mazuri na mikopo ya kidunia ni kujiingiza kwenye matatizo. Credit Economy haimuaji mtu Salama... hilo halihitaji wala kuingiza mambo ya Imani sababu wenye Imani zao watakwambia ya Kaisari muachia Kaisari....
 
Kwakuwa hutumia BIBLIA na Quran kuapa,

Lazima wayaelewe haya.

Mikopo ni fedheha.
 
Kwakuwa hutumia BIBLIA na Quran kuapa,

Lazima wayaelewe haya.

Mikopo ni fedheha.
Kwanza hivi huko tunapokwenda tunakopeshwa au tunabadilisha Almasi zetu kwa kupewa mawe na kushangilia kama Mazuzu......
 
Kwanza hivi huko tunapokwenda tunakopeshwa au tunabadilisha Alamasi zetu kwa kupewa mawe na kushangilia kama Mazuzu......
Wanaweka rehani almasi zetu, dhahabu, bandari na ardhi yetu.
 
(Mithali 22:7)
Akopaye ni mtumwa kwake Yeye akopeshaye!!

Nakusalimu popote ulipo Mh Ndugai.
Kwa hiyo sisi tuko sahihi kukataa mikopo na kufuata maandiko kuwa Riba ni haram?
Ila kuna watu wanaamini eti ooh hata matajiri hukopa
Kila mmoja ana nafsi yake
Mimi bora nidundulize miaka kufikia lengo kuliko kukopa

Kukopa ni umasikini wa akili na laana haswa
Hawa waizi wa mali ya umma wametoka kwenye umasikini na daima masikini haijui thamani ya hela ndio maana anaiba zote
 
Ninyi mnakataa mikopo yenye riba ila mnakubali kukopa mikopo isiyo na riba,

Inatakiwa ukopeshe, Si uwe mkopaji.

Mfumo wa kuanzisha biashara Kwa kuweka raslimali zako kama nyumba na mashamba ni mfumo ovu, mfumo huo unahamishia Mali zako ziende Kwa wakopeshaji.

Mfumo huo unakulazimisha uwakamue hasa wanunuzi Ili upate faida itakayotumika kulipa Riba, Kodi ya Pango, Kodi ya sirikali, mishahara, na mkopo wenyewe,Bado hujalisha family Yako nk nk!!

Mwisho wa siku, unakuwa tajiri usiyelala USINGIZI,

Unazidiwa na msukuma mkokoteni anayelala USINGIZI usio na stress ndani yake.

Usikope, kopesha ikiwa u Mbarikiwa.

Mkuu hapo kukopa mikopo ya bila riba pia ina walakin maana bado utalipa tu cha juu yaani wanahalalisha riba

Kuhusu kukopesha nimkopeshe nani wakati hazirudi 😄 hebu nielewwshe labda sijaelewa maana halisi ya kuwa mkopeshaji as individuals
 
Mtu akija kukopa kwako, ikiwa unayo mpenusimzuilie.

Na usiweke moyoni kuwa ni LAZIMA akurudishie,

Ukimkopesha Kwa Imani, ni unamkopesha Mungu,

Mimi nimewahi wakopesha wengi na wakasema watarudisha lakini hawakurudisha,

Cha kushangaza ni kuwa, Mimi niliyekopesha sikupungukiwa chochote ninachohitaji, lakini niliowakopesha na wasirudishwe, taabu hazikuisha.

Nadhani umeona jinsi Mungu anavyofanya KAZI kuhusu Kutoa/ kukopesha.

Imeandikwa ni kheri Kutoa kuliko kupokea.

Katika Ulimwengu wa Roho, ukipokea kitu au msaaada Toka Kwa mtu katika mwili, mtu yule aliyetoa katika mwili, anapokea katika Roho Kutoka kwako.

Nimeona matajiri wengi waliogundua Hilo, Kila ijumaa hutoa pesa nyingi Kwa maskini, na Kwa kufanya hivyo, Mungu huhamisha baraka za maskini na kuzidi kumtajirisha tajiri maradufu Ili azidi kuwajali maskini.

Penda sana Kutoa/ kukopesha kuliko kupokea/ kukopeshwa, maana mambo hayo huenda vice versa!!

Ubarikiwe 🙏
 
Back
Top Bottom