Waliobarikiwa hukopesha, kamwe hawanuki madeni, tubadili mtizamo

Nashukuru kwa ufafanuzi wako, tangu mdogo nilikuwa naona wazazi wakitoa sana sio tu kukopesha hata sadaka wametoa sana na sisi tumeiga kwani hatukuona wamefilisika kwa kutoa
Na kweli wengi ambao wanakopa na hawarudishi au wenye tabia za hivyo huwa wanaishi maisha magumu kwa kukosa Imani

Ubarikiwe pia
 
Ni Kweli Kabisa,

Umenikumbusha,

NYUMBA za wachoyo Huwa haziishi shida na kupungukiwa,

Lakini nyumba za wakarimu, Huwa hakikosekani chakula hata waje wageni kumi Kila wiki.

Shetani amewashika WANADAMU hapo wasijue Siri Ili wazidi kuwa maskini.

Endelea kuwa mtoaji na hakikisha unawarithisha watoto na watoto wa watoto Siri hiyo Ili Umaskini usipate NAFASI katika malango Yako.

Amen
 
Hapo uliposema niendelee kuwarithisha watoto
Mwanangu mdogo kwa umri kaniambia baba naomba tukawaone Yatima kama last time nikamwambia nimeishaandaa hilo mtaenda na kuwapelekea zawadi na mtacheza nao kwa muda mtakao siku ya Eid

Ni utaratibu wa kila wakati na wanafurahia sana kuona watoto wenzao wakifurahi
Mungu awape roho ya Imani na kuwawazia wahitaji

Kuna siku niliona ajabu kubwa Kuna mwehu alikuwa amesimama anawaangalia watu waliokuwa wamekaa kijiweni bila kuongea anawaangalia nilipofika mimi akaniomba chakula
Jamaa mmoja akasema hata kichaa anachagua
Alikula akashiba
Wakati mwingine hata wao wanaona
Mungu ni mwema wakati wote na anaangalia waja wake
Ila kuna watu wanaona kutoa atafilisika au kwanini atoe
 
Loh kama Mungu amekujalia mtoto wa namna hiyo,

Umebarikiwa.πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…