Waliochaguliwa Umbwe High School

Waliochaguliwa Umbwe High School

Status
Not open for further replies.
Teh teh teh kwanza Hongereni kwa kuchaguliwa katika moja ya shule ngumu Tanganyika sijui kuhusu Zanzibar, ukimaliza hapa JKT huwezi kwenda kusumbuka coz hapa MTISAFI ni JWKBU(Jeshi la kupambana na wananchi wa kibosho Umbwe) naongea hivi kwasababu kupigana na wananchi wa kibosho kisa kugombea wanawake wa kibosho ni kawaida ila ukitulia ni kitu cha kusikia tu utaishi kwa amani mpaka unaondoka, ni utangulizi tu usitishike.
Sule inapatikana 20Km kutoka moshi mjini, ipo pembeni ya mlima mrefu Africa(Kilimanjaro), ipo katika mazingira mazuri ya baridi n ya kijani karibu muda mrefu wa mwaka ni mvua.Utakutana na wachaga wa Kibosho wanaozunguka shule ni wakarimu sana hasa wanawake zao na pia ni wazuri na chanzo cha ugomvi kati ya wanafunzi na wanakijiji ila inatokea mara chache sana. Utapanda gari Moshi mjini nauli ni 1000 au 1500 utashukia kituo kinaitwa KWARAFAELI na hapo utauliza njia ya kupanda kwenda shule kama 1Km hivi sio mbali nimekadiria.
Kitaaluma shule walimu wapo ila wakuungaunga kama unavyojua shul nyingi za kibongo, ila wanafunzi wanapigishana sana pindi wao kwa wao sitaki kuwadanganya kuwa hakuna walimu wapo ila ni wavivu kutimiza majukumu yao hasa katika kufundisha ila wanafunzi wanajua jinsi ya kuwahandle ndio maana migomo haiishi katika shule yangu kipenzi.
HudumA za chakula ni za kiserikali kama kawaida najua mtakuwa mmenielewa na ndio chanzo kikuu cha migomo yote iliyotokea nikiwa shulu na hata huu mgomo wa mwaka huu, ila misosi ya kununua ni kibao utakula ndizi mbivu mpaka usaze kuanzaia 50Tsh tuu sababu kibosho ni kama Jamaica kwa ndizi na mapalachichi matamu duniani yanapatikana hapa Kuanzia 50Tsh na kuendelea na akina mama lishe kama Mama Steve, Mama Lelo na mama Manka kuwa muangalifu wanatoa huduma za chakula mpaka kimwili angalia sana utakatwa mapanga bure.
Headmaster Mr Lyimo ndio kivuto katika shule kutokana na kutokuwa na msimamo kaita uongozi wake alishawahi kuruhusu watu wanywe Konyagi ili waache Viroba akizani Konyagi ni bei kubwa kwa hiyo wanafunzi hawawezi kununua kisha baadae akafuta kauli yake nisimzungumzie sana huyu mtu mtamuona wenyewe ni kituko aiseee.
Mazingra ni mazuri sana kwa kusomea, ilijengwa na wamishionari waKiingereza kipindi cha ukoloni na ipo karibu sana mlima Kilimanjaro na ni kivutio kikubwa utauna milima mzuri na barafu yake miaka yote utakayo kuwepo nilienjoy sana
MAHITAJI MUHIMU KISHURESHURE
Blanket kubwa maana kuna baridi kali aiseee na sweta kuna siku nzima hamuoni jua ni mwendo wa mvua bora ununue rainboot kuliko kiatu cha shule(Rainboot zinaruhusiwa) nunua kiatu cha kikamanda chenye kuhimli mikiki ya maji maana mvua ni nyingi ukununua cha kichina utaacha soli nyuma(HILI NI MUHIMU) pia kuna tope sana ndio maana nashauri boot.
Siku za Jumamosi kama kawaida mtakuwamnaibuka kwenye soko moja maarufu linaitwa Kombo ni skiku ambayo watu wote wa kibosho umbwe na maeneo ya jirani kama Lyamungo wanaibuka kupata mahitaji yao ya wiki nzima, huwa vijana wa Umbwe wanaenda kuvizia watoto wazuri si unajua kipururu kili 7 cha uboys tena lazima maaeneo kama haya uende vinginevyo vijana watadondokadondoka ovyo kama shule za girls so kombo ni muhimu usiache kwenda hasa msimu wa Christmass wachaga wakiwa wamerudi likizo kuna kuwa na sherehe nyingi na msosi huwa unakuwa free off charge usimiss sehemu hizi kutoa shombo za dona maharage.
Kwa ujumla ni sehemu nzuri kwa kusoma pamoja na matatizo machache ya Waalimu, wakati sisi tunaondoka(2012 February) walimu wengi walikuwa wameajiliwa naona wanajitahidi kupamba na hilo tatizo sababu limeleta migomo mara 3, nyie wengine mnaweza mkafaidi kutokana na harakati zete Maveteran wa kipindi cha nyuma hata msosi umeimprove kwa ubora.
Ni hayo tuu nadhani baadhi ya maelezo yatakufanya uelewe undana wa shule mengine utayaona ukifika performance ipo juu kama kawaida watu hawafeli ovyo labda ujiingize kwene makundi ya wanywa MBEGE,UGORO na Kitu Cha Chuga utapotea kwa uzoefu kama Veteran wa pale wngi wamepotea kupitia vitu hivyo na mapenzi watu wameacha watoto zao kijijini, wakaacha kusoma wakahusudu Uchi matokeo yake wakataga(SCORE 0) maana akina manka ni wazuri si unajua watoto wa kichaga tena kuwa muuangalifu utakatwa mapanga na baba zao hawana mchezo. Nitapita maeneo hayo kuja kuchukua cheti changu October hii kazeni na pia karibuni UDOM.

From
UMBWE VETERAN
View attachment 101813View attachment 101814

Umenikumbusha mbali sana...Pande za kwa Rafaeli then unapita Mlama Hadi Mti Safi...Aksante kwa picha, nadhani usafi bado kipaombele...Heat Room bado ipo?

 
du naenda kunenepa uko.kuna adi donat
Ni wewe tu,maisha cheap sana ---- chalii angu mmoja alitumia 1000 term nzima nimwendo wa kula ndizi na mapalachichi ya shule na unaweza usitumie hata bati ukiwa kiongozi wa chakula(anaumaarufu kuliko hata headboy)utakula vizuri mpaka basi watu wanatoka vitambi wakipata nafasi ya kuwa viongozi wa msosi ila inalawama sana hasa wanafunzi wakikosa msosi kuna raia wanatoka Mbeya na Kanda ya Ziwa wanapenda sana kuwa viongozi wa jiko.
 
katizi na fongo, Gwakisa umenikumbusha mbali sana, umbwe 1993 - 1996. Umbwe juu Ucheche sana hakuna kufeli enzi hizo
 
hahaha umetisha xana mkuu

Nilikkuwa pale 2008-2010 ECA. Ishu ya UMBWE vs LYAMUNGO nilishiriki. Ilikuwa ni bonge la vita ktk life langu aliye fariki alikuwa mdogo wetu frm mbeya.
Mnaosoma hapo fanyeni kumaintain peace aisee maana ile ilikuwa ni bonge la vurugu ukibahatika kuniona nitakupa full detail. Hiyo ni balance b/d bado cjafika hata robo ya story kuikuta balance c/d.
 
nilikkuwa pale 2008-2010 eca. Ishu ya umbwe vs lyamungo nilishiriki. Ilikuwa ni bonge la vita ktk life langu aliye fariki alikuwa mdogo wetu frm mbeya.
Mnaosoma hapo fanyeni kumaintain peace aisee maana ile ilikuwa ni bonge la vurugu ukibahatika kuniona nitakupa full detail. Hiyo ni balance b/d bado cjafika hata robo ya story kuikuta balance c/d.

nipe mpaka double entry
 
We dogo umeongea 9 cha kumi umesahau ile deby yetu LYAMUNGO(machame) VS UMBWE(weruweru)

sasa hapa ndo kuna ile vita inayouaga raia mapanga,maslesha,mipin ya majembe hapa ndo mahali yake!!

Mimi nimepita Lyamungo lkn.

Teh teh umenikumbusha siku za graduation yani tuliwahi kualika Umbwe boys 15 tu kwenye graduu ya dini pale weruweru ila kiluchotokea robo tatu ya shule ilikuja pale lol ikawa kama mixture yani umbwe girls na boys kulikuwa na fujo mpk mlinzi akawafukuza na mwaka uliofata wakazuia Umbwe wasije wakaalikwa Old Moshi, Lyamungo ma Moshi tech lol.
 
Ila nyie Umbwe kwa tabia zenu sijui wale majirani zenu wa Mlama sekondari wale wakike kama wanakuwa safe lol!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom