Waliochangia matokeo ya kidato cha nne kuwa hivi

Waliochangia matokeo ya kidato cha nne kuwa hivi

Njaare

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2010
Posts
1,081
Reaction score
275
Wanajamvi naomba kuwasilisha maoni yangu kuhusu matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012. Maoni yangu yatajikita zaidi upande wa waliotumia nafasi zao vibaya na kusababisha matokeo haya.

1
Serikali ya chama cha mapinduzi

Wizara pamoja na idara zilizomo chini yake imeshindwa kabisa kuisimamia elimu. Shule nyingi hazina walimu na hata zile zenye walimu ukaguzi haufanyiki. Kwa muda mrefu imekuwa ikipuuza malalamiko ya walimu na kuwavunja moyo walimu ambao ni wadau wakuu wa sekta ya Elimu.

2
Mahakama ya Tanzania

Maamuzi yaliyofanywa na mahakama ya Tanzania kuwalazimisha walimu warudi kabla ya matatizo yao kushughulikiwa yamesababisha walimu kuendelea na mgomo baridi. Mahakama ilifanya uamuzi kwa manufaa ya wizara badala ya manufaa ya umma. Mahakama ilitakiwa itafakari kwa kina na kujua hali halisi kuwa unaweza ukampeleka punda mtoni lakini huwezimlazimisha anywe maji. Mahakama ilitakiwa iihoji serikali kuwa itahakikishaje kuwa mahakama ikiwaamuru walimu kurudi kazini itahakikishaje wanafanya kazi wakati hata walimu wenyewe wanajua kuwa ukaguzi haufanyiki?

3
Wazazi

Wazazi hatujapenda kuwajengea watoto wetu tabia ya kujitegemea na kujisomea.

4
Wananchi wa kawaida na Wabunge

Wananchi pamoja na wawakilishi wetu tumekuwa tukiona hali ya elimu nchini ikishuka tunakaa kimya. Tumekuwa tukisema ngoja tuone watakapofeli itakuwaje. Tumewaacha wabunge wetu wakipitisha bajeti na mwisho wa mwaka unakuta taasisi za elimu zimepewa chini ya robo ya bajeti walopangiwa na hakuna mtu anayehoji sii mwananchi wakawaida, si mbunge wa diwani.. Watoto wetu wamekuwa wakiishi kwenye hostel za kupanga mitaani. Hatujui ni wangapi waliopata maambukizi kutokana na kutafuta hela za kujikimu na kutokuwa na mwangalizi!

5
Wanafunzi

Wanafunzi wamehudhuria shule miaka mine (4) wengine wakiwa wanafundishwa wengine wakiwa hawana walimu. La kushangaza hawakulalamika wala hawajachukua hatua yeyote kujitafutia jinsi ya kufaulu. Wakati wa likizo huwa wanakutana na wenzao walotoka shule nzuri. Huu ungekuwa wakati mzuri wa kubadilishana learning material na kulekezana. Hawajui kuwa Elimu ni kwa faida yake yeye mwenyewe.
 
Pia wanasiasa kuingilia mambo ya elimu,mpaka kulazimisha watoto waliofeli darasa la saba wajiunge na kidato cha kwanza.
 
Back
Top Bottom