Habari zenu wana-JF! Natanguliza heshima mbele.
Ndugu zangu, wengi wetu huwa tunategemea kupata taarifa kupitia mtandao huu wa kijamii kutokana na umaarufu na uhakika wa taarifa zinazowekwa hapa jamvini.
Mwezi April 18-21 kulikuwa na Interview kwa nafasi mbali mbali zilizotolewa katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa na Nachingwea. Mimi nilikuwa ni mmoja wa watu waliofanya Interview pale Maktaba Complex-Dar, Nilikuwa naomba kupata taarifa kutoka kwa wana JF kama tayari wameshaita kazini au bado na kama bado je inaweza kuchukua muda gani?
Shukrani zangu kwa wote mtakaoweka taarifa hapa.