Waliofeli kidato cha nne 2012 kujiunga kidato cha tano 2013

ISMAIL MKIMBIZI

Senior Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
192
Reaction score
23
Kufuatia matokeo mabaya na ya kusikitisha sana kwa mara ya kwanza Tanzania zaidi ya watahiniwa 60% kufeli, kuna mkakati unapangwa kuishauri serikali kupitia wizara husika kuwachagua wale wote waliopata DIV IV za point 26 na 27.

Akisimulia habari hizi, mmoja wa wajumbe wa tume ya Mh Waziri Mkuu Bw Mizengo Pinda inayofuatilia kujua nini kilichojiri kupelekea kufeli sana wanafunzi mwaka 2012 alisema " Hakuna jipya chini ya jua, kila kitu kipo wazi cha msingi ni serikali kuupokea ushauri huu na Wizara husika itekeleze"

Aliendelea kufafanua kuwa kama wangefauru nafasi zingejazwa sasa kwa kuwa hawakufauru ziko wazi na ni busara ya namna ipi itumike kujaza nafasi hizo kama si kuchagua wenye DIV IV point 26 na wasichana wa IV point 27? "Mwaka jana waliofeli na waliopata alama za chini darasa la saba walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2013 kwa nini wasifanyiwe hivyo hawa wa Sekondari ?" Alihoji.

Imeelezwa kuwa tume ilshatoa taarifa yake kwa Mkoa wa Da es Salaam na kuna wanasiasa wenye nguvu serikalini wako wanashauri kutokana na majibu ya TUME YA PINDA, basi serikali ichukue uamuzi huo wa kuwaunganisha wenye pasi hizo na wenzao kidato cha tano na vyuo mbalimbali.

Nilipotaka kujua kama kweli kuna uwezekano na itakuwa wazi kwa kupopea barua maalum au kufuatilia wizarani kirushwa rushwa alifafanua kuwa " Hii ni Tanzania bwana wanasiasa wenye nguvu wakiamua jambo kwa lengo fulani kila kitu kinawezekana kwa ulaini tu bila rushwa wala nini..."

Chanzo: Mjumbe Tume ya Pinda.
 
wajiandae kuunda tume nyingine kuchunguza matokeo ya wahusika hawa watapomaliza form six garbage in garbage out.
 
Waliopata four ya point 26 na 27 hawapo kwenye kundi la zaidi ya asilimia 60 waliopata sifuri.
 
natamani niwe hai 2016 nione results za mjukuu wangu mpendwa
 
Safi sana! Hii ndo serikali sikivu!
 
Enzi zetu waliofeli walikuwa wanaenda private schools(UTASIKIA KAFELI HUYO ANASOMA SEKONDARI YA PRIVATE) . Siku hizi wasio na uwezo ndo wanenda Governrment schools.
 
Mkuu unajua maana ya waliofeli? Tembelea shule za private uone watu wana div 4 za point 26 hadi 27 wansoma Alevel ila cha muhimu kinachozingatiwa ni zile C 3, Pia kuwa vijana wenye Div 3 lakin hawana C 3 na hawasomi Alevel.
So hapa wizara inachopanga kufanya ni kushusha alama atleast atakayejiunga na A-level awe na Credit 2 yaani C 2 na D pass 3.
 
Waliopata four ya point 26 na 27 hawapo kwenye kundi la zaidi ya asilimia 60 waliopata sifuri.

Zaidi ya 60% ni ziro, lakini kefeli sio zero pekee mfano gari lilipaswa kuvuka mlima kitongo likashindwa wakati wa kupanda likasimama na vigingi vikawekwa jibu ni limefeli, 26,27 hiyo na lile linalopaswa kumaliza mlima na kuishia kati likarudi nyuma na kupinduka jibu limefeli na kupinduka ziro hiyo. Je ikiwa wazazi wa wenye 26,27 wako wanahangaika kutafuta shule na vyuo mbalimbali kwa jitihada zao binafsi huoni kuwa wamefeli?

Na kama suala ni zaidi ya asilimia 60% kuwa four hizo hazimo ukijumlisha na hizo four inaweza kufikia hata 80% bado ni kufeli tu. Kama bado una swali nipo online nitakujibu kiualimu zaidi ya serikali iliyokufikisha hapo ulipo.
 

Point yangu ni kwamba hata hao waliopata four wakichaguliwa kujiunga na form five bado tatizo litakuwa pale pale kwa sababu zaidi ya asilimia 60 wamepata sifuri na hawatajunga na form five.
 

Mkuu failure is not a dirty word, any examination system must involve failure, examination which involves no failure is a peculiar one. Kilichopo hewani ni kufeli kufikia lengo, ambapo kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Taifa mtahiniwa anakwenda kufanya mtihani ikiwa kama mkataba fulani na Baraza na Serikali kupitia wizara husika ya kwamba ukifaulu kwa kiwango hiki utaendelea na masomo ukichaguliwa shule za serikali vyuo nk.

Hivyo basi kwa kuingia chumba cha mtihani wa NECTA elewa lengo ni hilo nililokuambia ikiwa mtu ana malengo tofauti hiyo ni juu yake ki - private private. Kufeli sio neno baya wala waliofeli sina maana kwamba hawana akili cha msingi ni kwamba yaliyokuja kwenye mtihani wakayakosea hawakuyaelewa vizuri wangeletewa wanayoyaelewa vizuri wangefaulu. Kwa hiyo anakuwa ameshindwa (amefeli mkataba) na sio kwamba hana akili.

Mfano, hujawahi kuona darasani mtu mnayemwamini anafeli somo fulani na yule msiyemwamini anafanya vizuri zaidi yake? Na haujawahi kuona unayemwamini darasani katika mtihani fulani maswali aliyoyakosa usiyemwamini ameyapata. Let say yule usiyemwamini maswali aliyoyapata yangekuwa kwa idadi hiyo hiyo ndio mtihani yule unayemwaminia si anakuwa amefeli lakini ana jiweza? Kufeli sio kutokuwa na akili na kwenda privete ni sawa waweza kupafomu zaidi hata ya waliofaulu NECTA, lakini mada inabaki pale pale NECTA 2012 ulifeli.
 
Point yangu ni kwamba hata hao waliopata four wakichaguliwa kujiunga na form five bado tatizo litakuwa pale pale kwa sababu zaidi ya asilimia 60 wamepata sifuri na hawatajunga na form five.

Yes Mkuu tupo pamoja nilidhani una ni disqualify kwa kichwa cha habari nilichokipandisha hapa jukwaani. Sorry kwa kukumiss understand siku nyingine ongeza details.
 
Reactions: EMT

Kwa tafsiri hiyo nimekuelewa mkuu.
 
Yes Mkuu tupo
pamoja nilidhani una ni disqualify kwa kichwa cha habari
nilichokipandisha hapa jukwaani. Sorry kwa kukumiss understand siku
nyingine ongeza details.

hawa waliopata dv 4 wange resit maana wakipelekwa form five,wale wa mwakani watakaopata dv 4 wataanza kudai nao wafanyiwe hivo.
 
hawa waliopata dv 4 wange resit maana wakipelekwa form five,wale wa mwakani watakaopata dv 4 wataanza kudai nao wafanyiwe hivo.
mhhhh! Kazi kweli kweli elimu yetuwanasiasa wanaipiga danadana.elimu ya msingi wameiua sasa wanataka na elimu ya sekondary mwishowe hadi elimu ya juu
 
mhhhh! Kazi kweli kweli elimu
yetuwanasiasa wanaipiga danadana.elimu ya msingi wameiua sasa wanataka
na elimu ya sekondary mwishowe hadi elimu ya juu

hii ndo serikari yetu inavyo pelekwa kama gari bovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…