ISMAIL MKIMBIZI
Senior Member
- Jan 13, 2013
- 192
- 23
Kufuatia matokeo mabaya na ya kusikitisha sana kwa mara ya kwanza Tanzania zaidi ya watahiniwa 60% kufeli, kuna mkakati unapangwa kuishauri serikali kupitia wizara husika kuwachagua wale wote waliopata DIV IV za point 26 na 27.
Akisimulia habari hizi, mmoja wa wajumbe wa tume ya Mh Waziri Mkuu Bw Mizengo Pinda inayofuatilia kujua nini kilichojiri kupelekea kufeli sana wanafunzi mwaka 2012 alisema " Hakuna jipya chini ya jua, kila kitu kipo wazi cha msingi ni serikali kuupokea ushauri huu na Wizara husika itekeleze"
Aliendelea kufafanua kuwa kama wangefauru nafasi zingejazwa sasa kwa kuwa hawakufauru ziko wazi na ni busara ya namna ipi itumike kujaza nafasi hizo kama si kuchagua wenye DIV IV point 26 na wasichana wa IV point 27? "Mwaka jana waliofeli na waliopata alama za chini darasa la saba walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2013 kwa nini wasifanyiwe hivyo hawa wa Sekondari ?" Alihoji.
Imeelezwa kuwa tume ilshatoa taarifa yake kwa Mkoa wa Da es Salaam na kuna wanasiasa wenye nguvu serikalini wako wanashauri kutokana na majibu ya TUME YA PINDA, basi serikali ichukue uamuzi huo wa kuwaunganisha wenye pasi hizo na wenzao kidato cha tano na vyuo mbalimbali.
Nilipotaka kujua kama kweli kuna uwezekano na itakuwa wazi kwa kupopea barua maalum au kufuatilia wizarani kirushwa rushwa alifafanua kuwa " Hii ni Tanzania bwana wanasiasa wenye nguvu wakiamua jambo kwa lengo fulani kila kitu kinawezekana kwa ulaini tu bila rushwa wala nini..."
Chanzo: Mjumbe Tume ya Pinda.