waliofeli kidato cha nne waula ufaulu sasa waongezeka....

waliofeli kidato cha nne waula ufaulu sasa waongezeka....

ndupa

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2008
Posts
4,403
Reaction score
148
Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa
waliofaulu mtihani wa kidato cha nne
mwaka jana imeongezeka kwa kati ya
asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta), kufanya
marekebisho alama za viwango vya
ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata
zinasema matokeo hayo ambayo
yamewezesha kiwango cha ufaulu
kupanda na kufikia asilimia kati ya 54
na 57, huenda yakatangazwa wiki hii
pamoja na yale ya kidato cha sita
ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta
kimesema matokeo hayo mapya
yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia
daraja la kwanza hadi la nne
umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa
matokeo yaliyotangazwa awali na
huenda yakafikia asilimia 57. Hii
inamaanisha kwamba watahiniwa
wapatao 82,000 ambao awali walikuwa
wamepata sifuri katika matokeo ya
awali sasa wamepanda na kupata
madaraja ya ufaulu katika matokeo
mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa
mwaka 2012 watakuwa wamefanya
vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao
watahiniwa 225,126 sawa na asilimia
53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani
huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi
alisema upangaji wa matokeo hayo
ulikuwa bado unaendelea.
“Ninachojua kwa sasa ni kuwa
mchakato unaendelea na matokeo
yatatangazwa mapema tu ili watoto
waweze kujiunga na shule mapema,”
alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani
ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa
yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa
367,756 waliofanya mtihani wa kidato
cha nne mwaka jana, waliokuwa
wamefaulu kwa daraja la kwanza
mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa
na asilimia 6.4. Waliopata daraja la
nne walikuwa ni 103,327 sawa na
asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa
240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata
sifuri, hesabu ambayo imebadilika
katika matokeo mapya ambayo
yanaonyesha kuwa sasa waliopata
daraja hilo ni 158,100 ambayo ni
asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta
zinasema kuwa licha ya kuwezesha
kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi
ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo
hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi
2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa
na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja
na wale wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake,
walikutana mwishoni mwa wiki
iliyopita kukubaliana masuala
mbalimbali juu ya matokeo hayo
pamoja na suala la matokeo ya
wanafunzi hao 2,500 kabla ya
kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile,
busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna
mwanafunzi ambaye alama yake
itashuka, kwa kawaida isingewezekana
mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa
amefaulu leo umwambie ameshuka,”
 
wayatangaze mapema vijana wanaBp! Zinapanda na kushuka
 
Back
Top Bottom