Walioigiza sauti ya Rais wa Kenya na kufanikiwa kuiba wakamatwa

Walioigiza sauti ya Rais wa Kenya na kufanikiwa kuiba wakamatwa

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
Source: Walioigiza kuwa rais wa Kenya wakamatwa

Polisi nchini Kenya wamewakamata watu saba wanaodaiwa kushirikiana kuigiza sauti ya rais Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali katika kumuibia pesa nyingi mfanyabiashara tajiri nchini humo -Naushad Merali.

Mmoja wa watu hao alimpigia simu Bwana Merali, ambaye ni mwenyekiti wa Sameer Africa, akiigiiza sauti ya rais Uhuru kenyatta akimshawishi ampatie pesa za kusaidia mipango ya biashara, kulingana na polisi.

Fedha kamili zilizoibiwa bado hazijafahamika wazi - mtandao wa habari wa gazeti la Daily Nation news umeelezea kuwa zilikuwa ni shilingi milioni 10 ($100,000; £76,000) huku gazeti la Star likisema pesa hizo zilikuwa ni shilingi milioni 80.

Saba hao walifikishwa mhakamani Jumanne, lakini bado hawajashtakiwa.

Polisi wamesema wanahitaji musa zaidi wa kufanya uchunguzi.

"kutokana na ugumu wa uchunguzi na idadi ya washukiwa wanaohusika , wakiwemo wale ambao bado hawajapatikana , uchunguzi unatarajiwa kujumuisha nyaraka nyingi zikiwemo zile za benki pamoja na uchunguzi wa kina wa data za mawasiliano simu ," ilieleza ripoti ya polisi iliyonukuliwa na gazeti la Daily Nation

Bwana Merali ni mmoja wa wawekezaji wakubwa nchini Kenya katika sekta mbali mbali ikiwemo teknolojia ya mawasiliano pamoja na makazi.

Mtandao wa The Sameer Group unasema kuwa Bwana Merali pia ni mjumbe wa Baraza la serikali la uboreshaji wa masoko ya nje pamoja na baraza la la uwekezaji.

Polisi iliwakamata washukiwa tarehe 22 na 23 Februari.

Wakati wa operesheni hiyo, polisi walikamata magari aina ya Toyota Land Cruiser, Toyota Mark X , Toyota Axio na Toyota Crown.

Uchunguzi huo unatarajiwa kubaini ikiwa magari hayo yana uhusiano na uhalifu huo.

Bwana Merali na rais Kenyatta bado hawajazungumzia juu ya tukio la kukamatwa kwa watu hao.
 
Bongo hapa mwezi wa 4 mwaka jana , watu walitumia advantage mwakyembe alivosema wote wanamotumia majuto kwenye matangazo mikataba ichunguzwe basi akavamiwa jamaa Mwenye neel salt watu wamevamia ofsn kwake na v8 2 na suti nyeusi, wakajitambulisha wanatoka state house wakidai wametumwa na mzee kuhusu mikataba ya majuto ili apate matibabu India basi ikapigwa simu ikaigizwa sauti ya jiwe muhindi akaanza kutetemeka akatoa dola elf80 wanaume hao wakaondoka kilaini kuja shtukiza kapigwa kilaini kabisa
 
Bongo hapa mwezi wa 4 mwaka jana , watu walitumia advantage mwakyembe alivosema wote wanamotumia majuto kwenye matangazo mikataba ichunguzwe basi akavamiwa jamaa Mwenye neel salt watu wamevamia ofsn kwake na v8 2 na suti nyeusi, wakajitambulisha wanatoka state house wakidai wametumwa na mzee kuhusu mijataba ya majuto ili apate matibabu India basi ikapigwa simu ikaigizwa sauti ya jiwe muhindi akaanza kutetemeka akatoa dola elf80 wanaume hao wakaondoka kilaini kuja shtukiza kapigwa kilaini kabisa
Hahahaha duh aisee hahahahahah haha sana
 
Bongo hapa mwezi wa 4 mwaka jana , watu walitumia advantage mwakyembe alivosema wote wanamotumia majuto kwenye matangazo mikataba ichunguzwe basi akavamiwa jamaa Mwenye neel salt watu wamevamia ofsn kwake na v8 2 na suti nyeusi, wakajitambulisha wanatoka state house wakidai wametumwa na mzee kuhusu mikataba ya majuto ili apate matibabu India basi ikapigwa simu ikaigizwa sauti ya jiwe muhindi akaanza kutetemeka akatoa dola elf80 wanaume hao wakaondoka kilaini kuja shtukiza kapigwa kilaini kabisa
Dah [emoji2] [emoji1]Bongo balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom