Walioishi Morogoro na Mwanza kupi kuzuri?

Walioishi Morogoro na Mwanza kupi kuzuri?

Mwanza
Njo Mwanza Ujenge
Luchelele
Buhongwa
Nyamongolo
Buswelu
Rumara n.k

Kuja Ufanye Business Mwaloni tukuuzie mazao ya Ziwa ukutane na wakongo, Warundi, wakenya n.k
Utafanya kazi na makabila kama Wasukuma, wakurya, Wajita, Wahaya , Wakerewe, Wakara , Waha, Wachaga n.k

Utalima , utafuga , utanunua na kuuza bila shida liwe Duka au bidhaa zingine zozote mpk Madini.
Mademu pia wapo ww tu .
Karibu Mwanza ( Rocky City).
Naikubali sana Mwanza nimekaa pale zaidi ya miaka 10.
 
Asanteni Kwa majibu mazuri ambayo yamenifungua machoo
 
Moro manispaa uzuri wake ni hali ya hewa nq maisha yao ni kama ya dar the way wanavyo ishi uzuri wa pili ni karibu na dar kingine vyakula sio gharama sana Mwanza ni jiji la utafutaji wa hela kwa mtafutaji wa hela biashara mwanza pana faa sana kuliko Morogoro
 
Ni rahisi kuyaongea sana..mwanza maisha sio marahisi kabisa...bora morogoro
Sijawahi kufanya maisha Moro japo kila Q lazima nikatize mitaa hiyo.

Mwanza: Population ni kubwa, pana pesa za Madini, Ufugaji, Uvuvi, Kilimo + waajiriwa wa private and public sectors.. Watu wake bado hawana customer care nzuri (wekeza kwenye hili eneo), hali ya hewa nzuri na vyakula vinapatikana. Ukweli mwingine ni kwamba Mwanza town Wasukuma bado ni wengi na hawajachangamka sana, ni rahisi kupata faida kubwa kufanya biashara kwao.

Moro: Sidhani kama pana advantage zaidi ya Mwanza.

Wengine waongeze.
 
Ogopa watu waliozaliwa na kukulia vibarazani. Wao hawanaga hela ila ya kusasambua hawawezi ikosa. Moro hao
 
Mkuu hiyo niliona Buhongwa,mtu kawekewa Whatsup kailipia buku ishirini alafu kafurahiiiiiiiiii.
Wasukuma sijui wanashida gani, nimemuuzia MiFi kesho yake karudi anafurahi utadhani nimemuhakikishia ataingia peponi, akanipa na hela tena
 
Wadau kati ya hiyo mikoa ipi mzuri Kwa familia na makazi na biashara .

Wajameni siitaji majibu ya hovyoo kama mdomo wako ni mchafu sana kapige mswaki kimya a
Morogoro, 1. Kielimu, Kuna shule za msingi nyingi za wamisionari, Fransalian, Benard Bendel, Theresian, Capuchin, Precious Blood, Adventists, Lutherans, Muslims, Indians, n.k. Vyuo ndo usiseme. VETA, LITI, ardhi, Forests, Universities. Ni mji uliojaa wasomi, kila ukizunguka, au ukiwa kwenye daladala ukosi degrees, professors. Wanafunzi na n.k.
2. Usafiri, kutoka DSM au Dodoma to Morogoro usafiri 24 hours. Magufuli stands, Aboods, BMs, Al Saids, uenda Morogoro kila dakika 15 zinatoka na zinajaa. Mabus 400 kwa siku ufanya Safari ya Dar - Moro na Dar - Dodoma. Acha Special Hire, au Mabus madogo ya Mbezi - Moro. SGR train itaanza inafunguliwa soon kwahiyo Morogoro itakua kama Brussels Belgium, watu wanajua na kwenda.
3. Kilimo na Chakula na Viungo, hapa Morogoro usijari. Vyakula kama Mashelisheli, Magimbi, Maboga, Iriki, Nazi, Kunde , Karafuu, Pilipili, Ndizi, Ufuta hivi vipo kwa Wingi hulimwa Morogoro DC(Milima ya Uluguru hasa Matombo), Mpunga, Miwa hutoka Tiriani, Ifakara au Malinyi, Viazi hutoka gairo na Mahindi hutoka Kilosa.
4. Hari ya Hewa. Morogoro hakuna mfano ukichoka na hari ya uvuguvugu unaenda Milimani kule Morning Site, au unaenda milima ya Uluguru Kuoga maji ya milimani.
5. Uwekezaji, fursa zipo, unaenda Morogoro DC kulima Ufuta, Karafuu, Iriki, au Unaenda Kilosa, mikese kulima mahindi au Unaenda Ifakara, mlimba, malinyi, Turiani,kulima Mpunga, au unasogea Gairo kulima Viazi. Unaweza baki mjini kuajiriwa viwanda vikubwa, au kujiajiri kwa kufungua biashara za electronics, migahawa, Utarii, Transport na nyinginezo.
6. Utarii, Morogoro kuna mbuga ya Mikumi, au unaweza enda Udizungwa(Sanje) au unaweza enda Nyerere National Park Kisaki(Morogoro DC), Ukapanda Milima ya Uluguru au ukaenda bwawa la Mindu, pia ukasafiri kwenda kwenye bwawa jipya la Umeme la Nyerere.
7. Fursa, miradi Mikubwa mingi ipo Morogoro, kuanzia bwawa la Nyerere, SGR train, Mgodi wa Madini wa Madini ya Kinywe(Australia), Scheme za umwagiliaji za zamani na mpya.
8. Viwanda vingi vya kilimo vipo Morogoro, pia nguo, sigara, mafuta, n.k. Pia ni Mkoa ambao bajeti kubwa ya serikali ya kilimo sehemu kubwa inaenda Mkoa huo hasa kwenye viwanda vya sukari kilombero, Mtibwa, Mkulazi na vingineo.
9. Muda, Ukikaa Morogoro utaweza kwenda Mkoa wowote ule kwa haraka bila kutumia nguvu. Muda ni mali na Maisha ni kutafuta. Morogoro hakuna kasumba ya wewe wa hapa au wakuja, utapewa ushirikiano popote, kwa kuwa vyuo ni vingi wananchi wengi wa Morogoro ni wasomi kimaisha, kila mtu anatafuta mkate Moro.
10. Malezi, Watoto wako watalelewa vizuri, kwa maadili, maana mchanganyiko wa jamii ni mkubwa na hakuna ushamba, ukabila wala udini.
Huu ni ushauri kwa mtazamo wa Morogoro, njoo tuijenge Morogoro, na ni haki yako kuishi popote. Ubatikiwe.
 
Back
Top Bottom