Wadau kati ya hiyo mikoa ipi mzuri Kwa familia na makazi na biashara .
Wajameni siitaji majibu ya hovyoo kama mdomo wako ni mchafu sana kapige mswaki kimya a
Morogoro, 1. Kielimu, Kuna shule za msingi nyingi za wamisionari, Fransalian, Benard Bendel, Theresian, Capuchin, Precious Blood, Adventists, Lutherans, Muslims, Indians, n.k. Vyuo ndo usiseme. VETA, LITI, ardhi, Forests, Universities. Ni mji uliojaa wasomi, kila ukizunguka, au ukiwa kwenye daladala ukosi degrees, professors. Wanafunzi na n.k.
2. Usafiri, kutoka DSM au Dodoma to Morogoro usafiri 24 hours. Magufuli stands, Aboods, BMs, Al Saids, uenda Morogoro kila dakika 15 zinatoka na zinajaa. Mabus 400 kwa siku ufanya Safari ya Dar - Moro na Dar - Dodoma. Acha Special Hire, au Mabus madogo ya Mbezi - Moro. SGR train itaanza inafunguliwa soon kwahiyo Morogoro itakua kama Brussels Belgium, watu wanajua na kwenda.
3. Kilimo na Chakula na Viungo, hapa Morogoro usijari. Vyakula kama Mashelisheli, Magimbi, Maboga, Iriki, Nazi, Kunde , Karafuu, Pilipili, Ndizi, Ufuta hivi vipo kwa Wingi hulimwa Morogoro DC(Milima ya Uluguru hasa Matombo), Mpunga, Miwa hutoka Tiriani, Ifakara au Malinyi, Viazi hutoka gairo na Mahindi hutoka Kilosa.
4. Hari ya Hewa. Morogoro hakuna mfano ukichoka na hari ya uvuguvugu unaenda Milimani kule Morning Site, au unaenda milima ya Uluguru Kuoga maji ya milimani.
5. Uwekezaji, fursa zipo, unaenda Morogoro DC kulima Ufuta, Karafuu, Iriki, au Unaenda Kilosa, mikese kulima mahindi au Unaenda Ifakara, mlimba, malinyi, Turiani,kulima Mpunga, au unasogea Gairo kulima Viazi. Unaweza baki mjini kuajiriwa viwanda vikubwa, au kujiajiri kwa kufungua biashara za electronics, migahawa, Utarii, Transport na nyinginezo.
6. Utarii, Morogoro kuna mbuga ya Mikumi, au unaweza enda Udizungwa(Sanje) au unaweza enda Nyerere National Park Kisaki(Morogoro DC), Ukapanda Milima ya Uluguru au ukaenda bwawa la Mindu, pia ukasafiri kwenda kwenye bwawa jipya la Umeme la Nyerere.
7. Fursa, miradi Mikubwa mingi ipo Morogoro, kuanzia bwawa la Nyerere, SGR train, Mgodi wa Madini wa Madini ya Kinywe(Australia), Scheme za umwagiliaji za zamani na mpya.
8. Viwanda vingi vya kilimo vipo Morogoro, pia nguo, sigara, mafuta, n.k. Pia ni Mkoa ambao bajeti kubwa ya serikali ya kilimo sehemu kubwa inaenda Mkoa huo hasa kwenye viwanda vya sukari kilombero, Mtibwa, Mkulazi na vingineo.
9. Muda, Ukikaa Morogoro utaweza kwenda Mkoa wowote ule kwa haraka bila kutumia nguvu. Muda ni mali na Maisha ni kutafuta. Morogoro hakuna kasumba ya wewe wa hapa au wakuja, utapewa ushirikiano popote, kwa kuwa vyuo ni vingi wananchi wengi wa Morogoro ni wasomi kimaisha, kila mtu anatafuta mkate Moro.
10. Malezi, Watoto wako watalelewa vizuri, kwa maadili, maana mchanganyiko wa jamii ni mkubwa na hakuna ushamba, ukabila wala udini.
Huu ni ushauri kwa mtazamo wa Morogoro, njoo tuijenge Morogoro, na ni haki yako kuishi popote. Ubatikiwe.