Waliojenga kibanda cha Mlinzi kwa Tsh. Milini 11 wafikishwa Mahakamani

Waliojenga kibanda cha Mlinzi kwa Tsh. Milini 11 wafikishwa Mahakamani

Nchi ya kulinda wezi
Ila panya roads wanapigwa risasi
 
Hakuna kesi hapo ni uzushi tuu wa kisiasa na watatoka vizuri tuu..

Kwani kibanda cha Mlinzi linatakiwa kuwa cha Bei gani?

Mwisho kumbe siku hizi makosa ya uhujumu uchumi huwa yanakuwa na dhamana?
Ndiyo uonevu huo wanaangalia na sifa ya mtu
Upumbavu kabsaaa
Kama yale ya padre Moshi
Kuna watu hizi Sheria haiziwagusi
 
Kabla ya kibanda hicho cha VETA cha milioni 11, zilitoka taarifa za idara flani ya maji( sikumbuki ni mkoa gani),wao walijenga kibanda kidogo zaidi ya hicho cha veta kwa milioni 13. Na wao wangemlikwa tu
 
Kwa jinsi manunuzi ya serikali yanavofanyika, kibanda kile kina thamani ya hiyo 11m au hata zaidi!!

Ni bahati mbaya waliolalamikia kibanda hicho na kusababisha mashitaka haya - ni wanasiasa. Ikifanyika BOQ, inawzekana kabisa pesa ambazo zitaonekana kuibwa sio zaidi ya 2m!!

Huduma au mali inazopatiwa serikali au taasisi za umma hutolewa kwa bei ya juu - sababu moja wapo ni ucheleweshaji wa malipo!! Unatoa huduma halafu unakaa miezi na hata mwaka ukisubiri kulipwa!!
 
Back
Top Bottom