Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Nimejenga nyumba ya room tatu kimoja master,.jiko ,dining , sitting, store na public ndan gharama had sasa Ni milion 15..na Bado sijaingia ndani..ujenz achen jamani..labda Kama Ni wa vyumba viwili..[emoji124]
 
View attachment 1789129
Huu ni mfano wa makadirio ya Gharama za msingi kwa nyumba ya vyumba vitatu. Hapo gharama za fundi hazijawekwa, Pia eneo likiwa na slope kidogo matofali yataongezeka na kifusi/mchanga
Broo mnajengea wapi ? Mbona kama umepigwa sana , ?
Nina project ya nyumba flan ya vyumba 3 vikubwa , inakaribia kwenye lenta tofali kutoka msingi nimenunua 2900 na zinaelekea kumaliza
Gaharama na ufundi hadi sasa zipo kwenye 5.7 mil
Sijapiga jamvi though maana hili laweza fanyika hata baada ya kupaua
 
Huu ni msingi wa gorofa au nyumba za kawaida? Na izo matofali 2500 ni za msingi wa nyumba ya vyumba vi ngapi? Kama ni nyumba ya vyumba 3 umepigwa mzee wangu... Mimi nina kwangu ila kila mtu huwa ananitajia bei anazojua yeye akiangalia nyumba yangu wanataja mahela mengi ila ukweli sijafika hata milioni 22
View attachment 1789129
Huu ni mfano wa makadirio ya Gharama za msingi kwa nyumba ya vyumba vitatu. Hapo gharama za fundi hazijawekwa, Pia eneo likiwa na slope kidogo matofali yataongezeka na kifusi/mchanga
 
Nimejenga nyumba ya room tatu kimoja master,.jiko ,dining , sitting, store na public ndan gharama had sasa Ni milion 15..na Bado sijaingia ndani..ujenz achen jamani..labda Kama Ni wa vyumba viwili..[emoji124]
Nyumba ya vyumba viwili,kiko,dining,store etc ina tofauti ndogo sana na ya vyumba vitatu.
 
Tofali hizo kwa msingi inawezekana iwapo eneo sio tambarare. Kuna jamaa amejenga foundation tu tofali 2000, eneo lake liko kwenye muinuko
 
Nimepigwa? Site nipo mwenyewe kuanzia asubuhi mpaka jioni, vifaa nimenunua mwenyewe. Kiwanja kilikuwa na slope kidogo, upande mmoja wa msingi una kozi 8 above ground tofali za kulaza. Mkanda nimezungusha nondo 4 nyumba nzima. Hizo tofali hazikufika hivyo ila zilikaribia.
 


Umeuona msingi wenyewe?
 
Msingi wako sio wa kawaida ndio maana wengi wameshangaa.
 
Unataka nikuwekee na Ramani, Mimi siyo muuza ramani. Huu ujenzi ni wa kwangu na hayo ndio makadirio niliyowekewa na mchora ramani
Ni sawa na mimi niseme gharama za usafiri ni shilingi 50,000/-

1. Nauli 40,000/-
2. Chakula njiani 10,000/-

Nauli ya kwenda wapi?
Kutokea wapi?
Kutumia usafiri gani?

Ukisema hizo ni gharama za msingi wa nyumba ya vyumba vitatu. Vina ukubwa gani? Sebule ukubwa wake, jiko, vyoo, milamgo ma madirisha mangapi? etc...
Bila hivyo unakuwa kama umesema tu, halafu?
 
Yani watu wanajua kutishana asee, nyumba yangu ya kwanza ilitumia matofali 2600 hadi juu
Vyumba 3 sebule dinning choo public na jiko
inategemea na eneo
binafsi msingi ulikula tofali 2400
 
Madirisha yanahusianaje na msingu mkuu? Material makaridio ndio hayo niliyoweka hapo na ni ya hatua ya msingi pekee, Kama hukubaliani nayo haina shida nimetoa mfano tu. Pia naona bora mchora ramani aki overestimate material kuliko aka under estimate.
 

Ujenzi wa nyumba ni gharama kutegemea na wewe mjengaji, ni kama vile kumiliki gari au simu. Sio kila nyumba iko sawa na nyingine. kuna nyumba ya gharama na nyumba mradi nyumba. Kwa hiyo Nichumu Nibebike wala usiogope.
 
La maana uwe na kiwanja! Anza kununua vitu taratibu, jiulize akina mama waliojenga kwa kuuza maandazi walifanyaje?
 
Madirisha yanahusianaje na msingu mkuu?
Dead load ya jengo. Msingi si lazima ujue jengo lina uzito kiasi gani?
Labda kwa udongo na ukubwa wa jengo lako unahitaji Nondo nne au sita za 16mm.
Au labda unahitaji footings zilizo isolated etc..
Bila ramani ujumbe unakuwa kama haupo kamili. Anyways, yaishe sikuwa na nia mbaya.
 
Mwambie akajenge Kariakoo au posta ndo ataelewa... Anataka kufananisha gharama ya nyumba hiyo hiyo kuanzia kiwanja, iliyoko posta DSM na iliyopo Malinyi
 
Acha kudanganya watu labda kama unajenga kibanda kijijini ila ujenzi ni gharama, take it from me.

Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app
Ni gharama hasaaaa lakini ukimwambia mtu ukweli anadhani unamdanganya au unajisifia.

Kabla ya kuanza ujenzi, jaribu kununua daftari na uweke gharama zote za ujenzi ambazo utazitumia. Pale utapomaliza basi piga hesabu ya matumizi yako.

Kwa kweli hutaamini kwamba ulitumia fedha zote zile kwenye ujenzi.

Shida yetu sisi huwa tunajenga pole pole, leo laki mbili kesho laki nne kadiri unavyopata fedha na kuliendeleza jengo pole pole. Lakini piga gharama zote uone huo mchezo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…