Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Mimi nimejenga chumba na sebule kila kitu.. basic finishing.. no tiles.. kwa 5m tu... ila kuna uzi humu watu walikuwa wanasema milion 10.. nikakata tamaa..

Nilivyokaza roho na kuanza ujenzi hadi nimehamia
 
kuna wale hawajawahi kununua hata mfuko wa cement ndio wanaosema ujenzi rahisi. Hata kama una kipato kizuri ujenzi ni gharama. Usione wenye nyumba wanatoa lugha ngumu mnapobamiza milango they know its price.
 
Nlitaka kujenga nyumba mkoa *****, mwenzangu akasema:-

"mmmh pale utaona wenzio wanaachia migorofa tu, we unabaki na ya kawaida, kwa nini usijenga hapa *********"

Tokea siku iyo akili imeganda .
 
kuna wale hawajawahi kununua hata mfuko wa cement ndio wanaosema ujenzi rahisi. Hata kama una kipato kizuri ujenzi ni gharama. Usione wenye nyumba wanatoa lugha ngumu mnapobamiza milango they know its price.
You made my day.... Watu hawashangai watu wanakimbia site wanaacha magofu...
 
mi nimejenga chumba na sebule kila kitu.. basic finishing.. no tiles.. kwa 5m tu... ila kuna uzi humu watu walikuwa wanasema milion 10.. nikakata tamaa..

nilivyokaza roho na kuanza ujenz hadi nimeamia
inatagemea na location na materials used, unaweza kujenga kwa tofali za kuchoma ukatumia mbao za bei nafuu kuezeka na madirisha ya bei nafuu pia. ila ujenzi ni finishing na hapo ndio kazi ilipo
 
Achaneni na immitation, mm nilianza na kazi ya kawaida kabisa early 2005 nikanunua uwanja. Ujenzi unauma! Uchungu! Hela yote inaishia kwenye nyumba hasa pale mafundi wamefikia kwenye finishing uko radhi hata usinywe soda.! Ilifika kipindi nikataka kuuza baada ya kuona saving inakuwa ndogo kila mwezi.. All in all jitose! Never give up! Kadri unavyojitavidi the more the trouble knocking on to you! Jikakamue
 
Kama ni mtanzania wa kawaida mwenye kipato cha halali kisichozidi milioni kwa mwezi huwezi kusema ujenzi ni rahisi. Tuliojaribu tunajua gharama zake. ukuta mpaka uwe safi kuna mafundi kadhaa wameupitia. Tena hapo umetumia local fundis sikwambii ukitaka wale wa kukukabidhi funguo.
 
Kama basic finishing ni floor ya cement tu na madirisha ya wavu labda.
mmmmh! hayo madirisha ya wavu ikija mvua ya upepo ni shughuli pevu. Ni bora hata kama ukashindwa yote lakini uweke vioo dirishani. Naamanisha hata chini uweke jamvi tu, hata ukose plasta/ripu, gipsam na mengineyo lakini madirisha kuwekewa vioo ni muhimu sana
 
dahhh!! nikiona hayo mamilioni mnayosema eti ndo gharama ya chini navurugwa tumbo, ama hakika ujenzi noma, ila kufikia mwaka 2020 lazima niwe kwenye mjengo wangu mzuuuri!!
Mungu akutangulie ndoto yako na dhamira yako itimie, inshallah!!
 
mi nimejenga chumba na sebule kila kitu.. basic finishing.. no tiles.. kwa 5m tu... ila kuna uzi humu watu walikuwa wanasema milion 10.. nikakata tamaa..

nilivyokaza roho na kuanza ujenz hadi nimeamia
Hongera mkuu. Kapicha tafadhali.
 
Upo sahihi sana, ila ujenzi hauna ghalama maalum. Kwa mfano kuna mtu anaweza kujenga nyumba kwa Milioni 70 na mwingine akajenga nyumba hiyo hiyo na kwa ramani hiyo hiyo kwa M100. Tofauti kubwa hapo ni nyumba unaijenga wapi na unafanyia finnishing vifaa gani na vya bei gani
 
Safi mkuu umekuwa objective.
 
unafikiri nyumba inajengwa kwa shilingia mia tano!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…