Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

mi nimejenga chumba na sebule kila kitu.. basic finishing.. no tiles.. kwa 5m tu... ila kuna uzi humu watu walikuwa wanasema milion 10.. nikakata tamaa..

nilivyokaza roho na kuanza ujenz hadi nimeamia
Mimi nimejenga nyumba vyumba viwili(vyote ensuite), sebule na jiko mpaka sasa hivi imefikia tzs 30m. Kuna vitu vichache bado vikikamilika mahesabu yangu yananiambia itafika tzs 35m. Kinachokula hela ni finishing mfano vifaa vya umeme switches/sockets ni chrome (imported) tiles nimeweka 60*60, 50*50 zikiwemo zile nyeusi. Madirisha as usual aluminium windows, fitted kitchen with work top plus all appliances, mosaic tiles ukutani,gypsum ceiling +lights,bathroom wall tiles from floor to ceiling,rangi ndani silk nje weather guard.

Kwahio inategemea umemaliziaje hata mimi ningeweza kujenga kwa 20m ikakamilika lakini kwa standard tofauti au gharama hii hii ningejenga ya vyumba vitatu au vinne kwa finishing tofauti.
 
Mleta mada upo sahihi. Kujenga ni simple kiasi.

We anza kununua material taratibu..... usikope kununua material, ila kopa kufanya finishing.

Waliojenga wana wanatisha sana watu.
 
Jamani wale mliopanga usibamize mlango wa MTU. Jana nimeshindwa kufanikisha azma ya kusafirisha milango yangu ya mjinga kutoka Tabora futari haikua tamu jana . Heshima kwa mababa wote wenye nyumba mjini
 
Ndio nyie tunaowazungumzia.
Nyumba ya mabati sabini kwa elfu kumi na tano bati moja ni milioni moja hiyo.
Mbao za milioni na nusu zinatosha kupaua.
Matofali elfu mbili na mia tano ni milioni tatu hiyo, cement ya kujengea mifuko mia ni sh milioni moja hiyo.. Fundi wa kujenga na kupaua, milioni nne hiyo.. Hizo gharama unazozungumza, unajenga shule?
Ha ha ha ha ha ha ha mkuu umenichekesha kwa kweli
halafu wengi wao wana story za kufanana hasa hasa watu wa makamo kati ya miaka 33 mpaka 40.
kuna jamaa flan hiv kajenga nyumba yake Kwa Mathias akamaliza fresh kabisa na kuhamia basi akifika maskani story zake zote ni gharama za ujenzi na kulalamika ujenzi umemmalizia pesa baada ya mwaka akaja mzee mmoja ni mhandisi wa Majengo na yeye akatoa kitu chake safi kabisa kupita kile cha jamaa.
Basi jamaa akaanza kutupa story nyumba ya mhandisi kwa makadirio ya chini ni mil 170, siku moja yule mhandisi akasogea maeneo ya maskani ikabidi watu tumuulize akasema imemgharimu mil 74 nyumba kuisha na akatupa evidence kuanzaia ujenzi unaanza mpaka unaisha yule jamaa akawa bado anang'ang'ania kiwango cha chini ni mil170
 
Ndio nyie tunaowazungumzia.
Nyumba ya mabati sabini kwa elfu kumi na tano bati moja ni milioni moja hiyo.
Mbao za milioni na nusu zinatosha kupaua.
Matofali elfu mbili na mia tano ni milioni tatu hiyo, cement ya kujengea mifuko mia ni sh milioni moja hiyo.. Fundi wa kujenga na kupaua, milioni nne hiyo.. Hizo gharama unazozungumza, unajenga shule?

Hapo ndipo unapovuja sasa...kila mtu anajenga kwa kutumia materials na vifaa anavyopendelea..mwingine anaezeka kwa vigae,mwingine bati za vipande za msouth na mwingine anaezeka kwa masufuria yetu tuliozoea...unategemea gharama zifanane!??mwingine uzio wake tu na mapambo aliyoweka ni gharama za nyumba kamili ya mtu mwingine.So ww kama umekuta mtu kajenga kwa 20 ml na issue ikakamilika hatujui kapataje materials,au katumia materials gani na nyumba yake ina quality na ukubwa gani.Ni hayo tu
 
Ukiwa na kiwanja, gharama ya nyumba ya vyumba vitatu, kwa basic finishing ni around 20M. With the same house some one will mention kuwa ametumia milioni mia! Utadhani kajengea mchanga wa makinikia.
Hahahahahah,hivi makinikia ni nini
 
Mleta mada upo sahihi. Kujenga ni simple kiasi.

We anza kununua material taratibu..... usikope kununua material, ila kopa kufanya finishing.

Waliojenga wana wanatisha sana watu.
Labda kama kila mtu ana kipato kama wewe.
 
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Utakuta nyumba ya mil.30 mtu anakwambia hii nyumba imenigharimu karibu mil.80....
 
mi nimejenga chumba na sebule kila kitu.. basic finishing.. no tiles.. kwa 5m tu... ila kuna uzi humu watu walikuwa wanasema milion 10.. nikakata tamaa..

nilivyokaza roho na kuanza ujenz hadi nimeamia
Thaafi! Wewe sasa ndio wa kuigwa mfano... Cha muhimu ni ko move in. Ukishahamia kwako zile kodi za laki mbili tatu za kila mwezi unazo save ndio zitafanya fininshing. Yani in the next two or three years nyumba inakuwa complete.
 
KWANZA CEMENT IMESHUKA BEI

NYUMBA HATA MILIONI MOJA UNAWEZA KUJENGA.. INATEGEMEA NA HADHI YA NYUMBA NA SEHEMU UNAYOJENGA
 
Kweli kabisa mkuu, yaani ukikomaa na mafundi hata laki tano unahamia kabisa....

MILIONI 20 KUNA MIKOA MINGNE UNAJENGA JUMBA LA MAANA,ILA USIMAMIE MWENYEWE,UKIJENGA KIBOSS NYUMBA YA M 20 UNAAMBIWA M 80
 
Ukiwa na kiwanja, gharama ya nyumba ya vyumba vitatu, kwa basic finishing ni around 20M. With the same house some one will mention kuwa ametumia milioni mia! Utadhani kajengea mchanga wa makinikia.
Kuna rafiki yangu kajenga vyumba 3 na sebule kumuuliza msingi bei gani akaniambia million 15 nikamuuliza fundi kwa siri akasema m 6
 
Back
Top Bottom