Waliojifanya "Usalama wa Taifa" Mbele ya DPP Wakutwa na Hatia, Walipa Faini na Kuachiwa Huru

Waliojifanya "Usalama wa Taifa" Mbele ya DPP Wakutwa na Hatia, Walipa Faini na Kuachiwa Huru

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Joshua Kamalamo (37) na Yahaya Kapalatu (31) kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh3.9 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kujifanya maofisa Usalama wa Taifa (TISS).

Akitoa hukumu hiyo leo Mei 30, 2023, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate amesema baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka Mahakama hiyo imeridhika pasipo shaka yeyote kuwa washtakiwa hao wamefanya kosa hilo.

Kwa mujibu wa Hakimu hyo, Mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo kwa kuzingatia kuwa washtakiwa hao ni kosa lao la kwanza kwa upande wa mshtakiwa Kamalamo yupo kwenye matibabu ya macho itampa adhabu kwa kuzingatia sheria.

"Kama Mshtakiwa Kamalamo ameweza kwenda hadi kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akijifanya wao ni maofisa wa TISS, ili iwe fundisho kwa wengine; lazima Mahakama hii itoe adhabu," alisema.

Kabate alisema mshtakiwa Kamalamo anakabiliwa na mashtaka mawili la kudanganya yenye ni TISS hivyo mahakama hiyo inamuhukumu kulipa faini ya Sh1.4 milioni au kwenda jela miaka miwili na shtaka la kujifanya yeye ni ofisa wa TISS anahumiwa kulipa faini ya Sh1.5 milioni au kwenda jela miaka miwili ambapo kifungo cha jela kinaenda kwa pamoja.

Alisema kwa upande wa mshtakiwa Kapalatu Mahakama hiyo imemuonea huruma kwa sababu alipigiwa simu na mshtakiwa Kamalamo akimuomba wakutane feri kivukoni ili amsindikize mahala fulani hivyo asingepigiwa asingeenda kwenye ofisi ya DPP.

Kutokana na hilo Mahakama hiyo inakuhukumu kulipa faini ya Sh1 milioni Kwa kosa la kujifanya maofisa TISS au kifungo cha miaka miwili jela. Alisema mahakama hiyo imeamumua kumpa adhabu hiyo ili asirudie tena anapopigiwa simu na kuambiwa aende sehemu fulani anatakiwa kuchukua tahadhari.

Hata hivyo, washtakiwa hao wamelipa faini hiyo wamekwepa kifungo cha miaka miwili.
 
Hawa watu bhana. Wengine miez mitatu na fine ndogo ndogo.

Anyway, ndio Tanzania hiyo.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Joshua Kamalamo (37) na Yahaya Kapalatu (31) kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh3.9 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kujifanya maofisa Usalama wa Taifa (TISS).
Hawa wameonewa sana hata hivyo,

Mwenzao Lengai Ole Sir Buyer ye aliachiwa tu huru bila faini yoyote Kwa kosa hili hili kujifanya Afisa Kipenyo.
 
Basi labda usalama kweli.

Kosa lao ni kutumia vibaya nafasi zao.

Hai make sense walipe Tu faini waachiwe
 
Nani anaweza kuhakiki kama kweli mtu ni afisa usalama au anadanganya?

Kwanza hata kazi yao inaruhusu kutoa kitambulisho mahakamani kwa ajili ya ushahidi? Au namba zao za usajili?

Hakimu kilaza. Hata DPP pia ni kilaza, kwa sababu hawajui maafisa usalama wote nchini.
 
Back
Top Bottom